(+VIDEO)Ombeeni mtoto wangu apone-Baba yake DJ Evolve azungumza

Muhtasari
  • Kwenye video iliyotolewa kwa vyombo vya habari, baba ya DJ Evolve alisema alikuwa na huzuni kusikia kwamba watu wangetamani kifo juu ya mtoto wake
DJ 1
DJ 1

Baba wa mcheza santuri  DJ Evolve John Orinda ameelezea kusikitishwa kwake na ripoti kwamba mtoto wake ameaga dunia

Kwenye video iliyotolewa kwa vyombo vya habari, baba ya DJ Evolve alisema alikuwa na huzuni kusikia kwamba watu wangetamani kifo juu ya mtoto wake.

"Chochote ninachosikia sio sawa, sio kweli. Nilishtuka kusikia ripoti kama hizo. Tunapoamka kila asubuhi, jambo la kwanza ni kumuona  mtoto wetu, kwa sasa anaendelea vizuri

Kila mtu anapaswa kumwombea tu, kwa sababu mmesema mnampenda, mwombee apone. Hivi sasa, maombi yenu yanafanya kazi Anaweza kukaa peke yake kwa muda wa saa moja, kisha hulala tena. Anaweza hata kukaa kwenye kiti kwa masaa 8. Tumuombee tu, alikuwa katika hali mbaya, lakini sasa anaendelea vizuri, "alisema John Orinda.

Ripoti juu ya kifo cha Evolve ziliibukana kuenezwa kupitia kwenye mitandao ya kijamii Jumanne saa sita.

Mara tu baada ya uvumi huo kuenea, sehemu ya Wakenya kumlaumu mbunge wa Embakasi mashariki Babu Owino.

Evolve alipatana na ajali yake mapema mwaka wa 2020, huku akilazwa hospitali kwa zaidi ya miezi 5 akipokea matibabu.

Hii hapa video akizungumza;

Baba yake mcheza santuri DJ Evolve, Felix Orinda amekana madai kwamba mwanawe ameaga dunia. #OngeaUsikike

Posted by Radio Jambo on Tuesday, June 8, 2021