BAHATI AFIDIWA

Eric azawadi Bahati Sh200,000 baada ya kupoteza udhamini wa KFCB

Bodi ya KFCB ilisema kuwa video za Bahati ambazo zilikuwa zinasambazwa mitandaoni zilikuwa chafu na zilikiuka sera za ushirikiano.

Muhtasari

•Kupitia mtandao wa Twitter,bodi ya KFCB inayoongozwa na mkurugenzi mtendaji Ezekiel Mutua ilisema kuwa video za Bahati ambazo zilikuwa zinasambazwa mitandaoni zilikuwa chafu na zilikiuka sera za ushirikiano.

•Tamasha ya kuzindua albamu mpya ya Bahati ‘Love like This’ ilifanyika siku ya Jumapili katika hoteli ya Trademark jijini Nairobi.

Ericko akimwangushia Bahati pesa siku ya Jumapili
Ericko akimwangushia Bahati pesa siku ya Jumapili
Image: Instagram

Mcheshi maarufu Eric Omondi(Erico) ametunuku mwanamuziki Bahati Sh200,000 ambazo alipoteza baada ya Bodi ya Uainishaji Filamu nchini Kenya(KFCB) kukatiza udhamini wake na msanii huyo.

Erico alimpokeza Bahati kitita hicho wakati wa tamasha ya kuzindua albamu mpya ya Bahati 'Love like this' akidai kuwa ni "kuunga mkono msanii mwenza" 

Kwenye video iliyopakiwa kwenye mtandao wa Instagram, Erico anaonekana kushika bunda la noti na kumuangushia Bahati wakiwa kwenye jukwaa.

"Babe okota hii kabla wachukue" Bahati anaskika akimwambia mpenzi wake Diana baada ya pesa zile kuangushwa.

Mapema wiki iliyopita , KFCB ilikatiza udhamini wa zaidi ya laki mbili kwa Bahati kufuatia video ya kibao “Fikra za Bahati” ambacho aliwachilia wiki iliyopita.

Siku ya Jumamosi, KFCB inayoongozwa na mkurugenzi mtendaji Ezekiel Mutua ilisema kuwa video za Bahati ambazo zilikuwa zinasambazwa mitandaoni  zilikuwa chafu na  zilikiuka sera za ushirikiano.

Wiki hii KFCB imeghairi uungaji mkono wa thamana ya zaidi ya Sh200,000 kwa mwanamuziki Bahati kufuatia kupakia kwa video ambazo zilikiuka makubaliano ya sanaa safi na sera za ushirikiano wetu. “ KFCB ilitangaza.

Bahati kwenye wimbo "Fikra za Bahati'
Bahati kwenye wimbo "Fikra za Bahati'
Image: Instagram

KFCB ilisema kuwa sio lazima sanaa iwe chafu kuhusisha ngono ili kuuza au kutumbuiza.

Sanaa safi ni ya kufaa kutazamwa na kusikizwa na familia nzima na inauzwa zaidi kushinda sanaa chafu na iliyooza.” KFCB iliandika.

Bodi hiyo pia ilitangaza kuwa haingejihusisha kwa namna yoyote na tamasha ya kuzindua albamu ya’Love like this’.

Hata hivyo, kutokana na video zinazosambazwa mitandaoni, timu yetu imeamua kukatiza usaidizi huo na kutojihusisha kabisa na tamasha ambayo imepangwa.” KFCB iliandika

Tamasha ya kuzindua albamu mpya ya Bahati ‘Love like This’ ilifanyika siku ya Jumapili katika hoteli ya Trademark jijini Nairobi.

Wasanii mashuhuri nchini Kenya ni miongoni mwa wageni waliohudhuria tamasha hiyo.