'Wanaume wa kenya ni 'Stingy'-Huddah Monroe

Muhtasari
  • Huddah Monroe afichua sababu hajawahi wachumbia wanaume wa kenya
Screenshot.from.2019.10.17.12.37.26
Screenshot.from.2019.10.17.12.37.26

Mwanasosholaiti na mfanyibiashara Huddah Monroe kupitia mtandao wa kijamii wa instagram, kitengo cha maswali na majibu amewafungulia mashabiki wake roho yake.

Huddah amedai kuwa wanaume ambao amewahi chumbia maishani mwake kutoka Kenya hawapendi kutumia pesa kwa wapenzi wao.

Yaani wanaume 'stingy'.

Mfanyabiashara huyo amekuwa akiishi nchini Dubai kwa muda huku akiendeleza biashara yake.

"Nimewachumbia karibu wanaume wote wa aina yote duniani.  Chinese, India lakini kwa hakika najua wanaume kutoka Asia sio wa ligi yangu

Katika Afrika mwanamume kutoka Nigeria ni kuwa na maumivu ya kichwa, sio wabaya kwa kujivinjari lakini sio wa kuwa kwa ndoa nao labda ukitaka kufa ukiwa na umri mdogo

Maisha ni kuhusu uamuzi, hao pia sio wa ligi yangu,wanaume wa Kenya wanaweza kuwa 'stingy' sana mimi napenda kutumia pesa

Mwanamume ambaye anaongea french huyo ni wangu na wa ligi yangu," Huddah Aliandika.

 

(Mhariri: Davis Ojiambo)