"Amekuwa akinitunza kama yai" Vera asema kuwa mumewe amekuwa akimtumikia

Mwanasoshalaiti huyo amefichua kuwa amekuwa kwenye mahusiano mengi mabaya hapo awali, mengine tusiyoyajua

Muhtasari

•Bae ndiye binadamu wa ajabu zaidi. Haswa  zaidi tangu tugundue kuwa tutakuwa na mtoto hivi karibuni. Katika safari yangu ya ujauzito, amekiuka na kunitunza kama yai. Sigusi chochote, anahakikisha kuwa nakula matunda kila siku. Ananilisha  cha lazima, ananipikia na anasugua miguu yangu” Vera alisema

Vera Sidika na Brown Mauzo
Vera Sidika na Brown Mauzo
Image: Instagram

Mwasoshalaiti Vera Sidika amemsifu mpenzi wake Brown Mauzo kwa kumtumikia wakati wa ujauzito wake.

Vera amethibitisha kuwa hajakuwa akifanya kazi yoyote pale nyumbani kwani mumewe amekuwa akimtunza kama yai.

Bae ndiye binadamu wa ajabu zaidi. Haswa  zaidi tangu tugundue kuwa tutakuwa na mtoto hivi karibuni. Katika safari yangu ya ujauzito, amekiuka na kunitunza kama yai. Sigusi chochote, anahakikisha kuwa nakula matunda kila siku. Ananilisha  cha lazima, ananipikia na anasugua miguu yangu” Vera alisema

Mwanasoshalaiti huyo ambaye alipata umaarufu mkubwa kufuatia kuhusishwa kwa wimbo wa P Unit, ‘You Guy’ , ameshukuru Mungu kwa kumpa bwana mzuri hata baada ya kupitia kwenye mahusiano mabaya.

Kweli Mungu alijionyesha wakati alikuleta maishani mwangu. Nimekuwa kwenye mahusiano mabaya zaidi, mengine hamukuyajua. Ila hayo hayakunizuia kupenda tena” Vera aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Ameapa kuwa hatawahi sita kumpenda mwanamuziki Brown Mauzo.

Hapo awali, Vera amechumbia takriban watu watatu wanaojulikana wakiwemo mwanamuziki Otile Brown, daktari Mtanzania Jimmy Chansa na Yommy Johnson kutoka Nigeria

Jioni ya Jumatano, Vera alisisimua mitandao baada ya kufichua kuwa alikuwa mjamzito. Hata hivyo, hakubainisha jinsia ya mtoto wake .

Ametangaza kuwa bado hajatambua jinsia huku akisema kuwa amekuwa akisubiria sana kujua.