Wanamitandao wampongeza Vera Sidika kwa kufichua ujauzito

Mwanasoshalaiti Vera Sidika na mwanamuziki BrownMauzo waliweka wazi kuwa wanachumbiana mwezi wa Sepemba mwaka uliopita.

Muhtasari

• Kati ya Wakenya mashuhuri waliompongeza ni pamoja na mwanzilishi wa Bonfire Adventures Simon Kabu.

• Kabu aliylfichua kuwa walikubaliana na Vera kuwa iwapo mtoto atakuwa wa kike, Kabu atampatia Vera laki moja na iwapo atakuwa wa kiume basi Vera atampatia Kabu laki moja.

Vera Sidika akifichua mimba
Vera Sidika akifichua mimba
Image: Instagram

Mwanasoshalaiti Vera Sidika na mwanamuziki Brown Mauzo walisisimua mitandao siku ya Jumatano baada ya kutoa tangazo kuwa wanatarajia mtoto wao wa kwanza hivi karibuni.

Watu wa  matabaka mbalimbali kutoka mataifa mbalimbali wameendelea kupongeza wawili hao kufuatia tangazo hilo ambalo wamekuwa wakificha mashabiki wao kwa muda sasa.

Kwenye video aliyopakia mtandaoni siku ya Jumatano, Vera aliweka wazi kuwa amebeba mimba.

Vera na Mauzo waliweka wazi kuwa wanachumbiana  mwezi wa Sepemba mwaka uliopita.

"Hatuwezi subiri kukuona" wawili hao waliandikia mtoto wao mtarajiwa.

Kati ya Wakenya mashuhuri waliowapongeza wawili hao ni pamoja na mwanzilishi wa Bonfire Adventures Simon Kabu aliyefichua kuwa walikubaliana na Vera kuwa iwapo mtoto atakuwa wa kike, Kabu atampatia Vera laki moja na iwapo atakuwa wa kiume basi Vera atampatia Kabu laki moja.

“Simo!! Kumbuka niko na video ya ushahidi. Ulibashiri kuwa atakuwa mvulana na ukaniahidi laki moja ikiwa atakuwa msichana. Ni heri ulete pea kwani mashabiki wangu hapa wanatazama" Vera alimjibu Kabu

Waigizaji mashuhuri ni baadhi ya watu waliowapongeza wawili hao. Soma baadhi ya jumbe za pongezi hapa.

Hapo awali, Vera amechumbia takriban watu watatu wanaojulikana wakiwemo mwanamuziki Otile Brown, daktari Mtanzania Jimmy Chansa na Yommy Johnson kutoka Nigeria ila hakujaliwa mtoto nao .

(Mhariri: Davis Ojiambo).