MAHUSIANO YA VERA SIDIKA

Kando na Mauzo, wafahamu wanaume waliowahi chumbia Vera Sidika

Muhtasari

Ni dhahiri kuwa mpenzi wake wa sasa, mwanamuziki Brown Mauzo, ndiye baba ya mtoto mtarajiwa.

•Vera alishangaza wanamitandao baada ya kufichua hadharani kwamba Otile hakuwa anamtosheleza kitandani. 

Vera Sidika na Brown Mauzo
Vera Sidika na Brown Mauzo
Image: Instagram

Siku ya Jumatano, mwanasoshalaiti Vera Sidika alisisimua mitandao baada ya kufichua kuwa amebeba ujauzito.

Vera alipakia picha na video zilizoashiria kuwa hatimaye atakuwa anajifungua mwanawe wa kwanza hivi karibuni.

Ni dhahiri kuwa mpenzi wake wa sasa, mwanamuziki Brown Mauzo, ndiye baba ya mtoto mtarajiwa.

Vera amemsifia sana Mauzo huku akimshukuru Mola kwa kwa kumzawadi mpenzi mwema maishani mwake. 

Mwanasoshalaiti huyo amesema kuwa Mauzo amekuwa akimtunza kama yai. Amefichua kuwa hajakuwa akifanya kazi yoyote pale nyumbani kwani mwanamuziki yule kutoka Pwani amekuwa akimtumikia.

Vera alifuchua kuwa hapo awali amechumbia wanaume ambao hawajamuonyesha mapenzi ya kufana.

"Nimekuwa kwenye mahusiano mabaya zaidi, mengine hamukuyajua. Ila hayo hayakunizuia kupenda tena" Vera alisema.

Kando na Mauzo, kunao wanaume ambao Vera anajulu

Otile Brown.

Vera Sidika na Otile Brown
Vera Sidika na Otile Brown
Image: Hisani

Vera na mwanamuziki Otile Brown walichumbiana mwaka wa 2018.

Wawili hao waliweka wazi uhusiano wao kwenye mitandao ya kijamii na kuonekena kufurahia uhusiano huo kutokana na picha na video walizopakia mitandaoni kila uchao.

Wawili hao walionekana kupendana sana kilele cha mapenzi kikiwa Otile Brown kumtungia wimbo 'Baby Love' ambao ulielezea mapenzi yake kwa mwanasoshalaiti huyo.

Hata hivyo, wawili hao walitengana baada ya kuchumbiana kwa miezi kadhaa. 

Vera alishangaza wanamitandao baada ya kufichua hadharani kwamba Otile hakuwa anamtosheleza kitandani. 

Uhusiano huo ulisaidia kuinua taaluma ya Brown ya muziki kwani baada ya yale kutokea, amekuwa ankivuma sana nchini na nje ya mipaka ya Kenya.

Jimmy Chansa Minja

Chansa ni daktari na mwanamuziki raia wa Tanzania ambaye walichumbiana na Vera mwaka wa 2019.

Wawili hao walipatana nchini Tanzania miezi kadhaa baada ya Vera kutengana na Otile Brown na kuanza kuchumbiana.

Vera Sidika na Jimmy Chansa
Vera Sidika na Jimmy Chansa
Image: Hisani

Hata hivyo, mapenzi yao hayakudumu sana kwani wawili hao walitengana mapema mwaka uliopita.

Vera alisema kuwa uhusiano wake na Chansa ulikuwa 'sumu'  na ndio maana wakatengana. Kwa upande wake Chansa alidai kuwa hana majuto yoyote kuwahi chumbia Vera.

Yommy Johnson

Vera Sidika na Yommy Johnson
Vera Sidika na Yommy Johnson
Image: Hisani

Vera aliwahi chumbia mwanasholaiti mzaliwa wa Nigeria, Yommy Johnson, ambaye alikuwa akiishi Dubai.

Wawili hao walichumbiana kwa muda kati ya mwaka wa 2016 na 2017.

Hata hivyo, wawili hao walitengana  huku kila mmoja akitoa sababu zake za kuacha mwingine.

Vera alisema kuwa Johnson alikuwa mtu mwenye vurugu na alimnyanyasa huku Johnson kwa upande wake akisema kuwa Vera aliavya mimba yake.

Daktari Badmus Tommy Daniel

Vera aliwahi chumbia mwana jinakolojia raia wa Nigeria kwa jina Badmus Tommy Daniel.

Ingawa sio mengi yanajulikana kuhusu uhusiano wa wawili hao, inaaminika kuwa mwanasoshalaiti Vera Sidika alichumbia daktari huyo kwa kipindi cha miezi kadhaa mwaka uliopita.

Hii ni baada ya kutengana na daktari mwingine, Jimmy Chansa, kutoka Tanzania.

Vera na Badmus ambaye pia ni mwanamitindo walionekana kubadilishana maneno matamu yakimapenzi kwenye mitandao na kuashiria kuwa walikuwa wanachumbiana.

Kwa sasa Vera ameweka wazi kuwa anafurahia uhusiano wake na Brown Mauzo. Wawili hao wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza hivi karibuni.