BURIANI BUNNY WAILER

Hatimaye mwanamuziki Bunny Wailer azikwa baada ya miezi 3

Mwili wa marehemu umekuwa umezuiliwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kwa kukosa hati ya mazishi kufuatia deni kubwa ya bili ya hospitali.

Muhtasari

•Wailer aliaga tarehe 2 mwezi Machi katika hospitali ya Medical Associates  alipokuwa anahudumiwa baada ya kuugua kiharusi mwezi wa Julai mwaka jana.

•Mazishi ya Wailer yalifanyika kwenye hafla iliyohudhuriwa na familia pekee kufuatia mikakati iliyowekwa na serikali ya Jamaica kudhibiti virusi vya Korona

Bunny Wailer
Bunny Wailer
Image: Hisani

Hatimaye mazishi ya Neville O'Riley Livingston almaarufu kama Bunny Wailer yalifanyiika siku ya Ijumaa, Juni 18, baada ya marehemu kuaga miezi mitatu iliyopita.

Mazishi ya Wailer yalifanyika kwenye hafla iliyohudhuriwa na familia pekee kufuatia mikakati iliyowekwa na serikali ya Jamaica kudhibiti virusi vya Korona.

Hata hivyo, hafla hiyo ambayo ilifanyika nyumbani kwa marehemu maeneo ya Dreamland  ilionyeshwa kwenye mitandao ya kijamii.

Umma haukukubalishwa kuona mwili wa marehemu kufuatia mikakati ya kudhibiti Covid 19.

Wailer aliaga tarehe 2 mwezi Machi katika hospitali ya Medical Associates  alipokuwa anahudumiwa baada ya kuugua kiharusi mwezi wa Julai mwaka jana.

Aliaga akiwa na umri  wa miaka 73.

Mwanawe Bunny Wailer akimpa babake heshima za mwisho
Mwanawe Bunny Wailer akimpa babake heshima za mwisho
Image: HISANI

Wailer alikuwa mwanzilishi pekee wa kikundi cha Wailers aliyekuwa amebaki baada ya waanziishi wengine, Bob Marley na Peter Tosh kuaga mwaka wa 1981 na 1987 mtawalia.

Mwili wa marehemu umekuwa umezuiliwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kwa kukosa hati ya mazishi kufuatia deni kubwa ya bili ya hospitali.

Inadaiwa kuwa familia ya marehemu ilikuwa na mzozo na kampuni ya kutengeneza muziki iliyowatataka kutia saini mkataba ili waweze kulipa deni ya hospitali.

Watoto wa marehemu waliweza kulipa deni ya hospitali karibia mwisho wa mwezi Aprili na kuanza shughuli za mazishi.

Buriani Bunny Wailer.