SIMBA KAWINDA MWINGINE

Simba awinda tena: Diamond amefichua kipenzi kipya

Mwanamuziki huyo kutoka bongo ameahidi kuwa atakuwa mwaminifu mara hii

Muhtasari

•Kupitia video aliyopakia mtandaoni wa Instagram, Diamond Platnumz almaarufu kama Simba amejionyesha akiwa na kidosho mwenye sura nyeupe pe pe pe  ingawa hajatambulishwa.

•Simba anajulikana kuwahi chumbia wanawake zaidi ya kumi kutoka mataifa mbalimbali kisha kuwatema. 

Diamond na Andrea Abrahams
Diamond na Andrea Abrahams
Image: Instagram

Je, Simba kapata windo lingine?

Baada ya kumtema mwanamuziki Tanasha Donna  kutoka Kenya, Diamond amewaacha wengi vinywa wazi baada ya kufichua hadharani anayesemekana kuwa kipenzi chake kipya.

Kupitia video aliyopakia mtandaoni wa Instagram, Diamond Platnumz almaarufu kama Simba amejionyesha akiwa na kidosho  mweupe pe pe pe ambaye anadaiwa kuwa mpenzi wake  ingawa hajatambulishwa.

Wawili hao walikuwa  wameandamana kwenye gari jipya la mwanamuziki huyo huku Diamond akiimba wimbo wake mpya ambao unasema amekuwa mwaminifu na ataendelea kuwa mwaminifu.

 

Siku za hivi karibuni, Diamond amekuwa akishukiwa kuchumbia mwanamitindo kutoka Afrika Kusini, Andrea Abrahams.

Ingawa wawili hao hawaonekana hadharani, wamekuwa wakiashiria ishara kuwa huenda wanachumbiana.

Diamond alipoulizwa kuhusu Andrea kwenye mahojiano na stesheni ya Wasafi FM, alisema kuwa amekuwa akimuwinda malaika huyo kwa muda mrefu sana.

" Yeye ni kamili, kamili sana. Anajua kuisha kwa amani na familia yangu bila drama yoyote" Diamond alisema.

"Nilianza kumchumbia mwaka wa 2013 akanizungusha na amekuja kunikubali mwaka uliopita" aliendelea kusema.

Alipokuwa anafichua kipenzichake kipya  hadharani siku ya Jumamosi, Diamond ameahidi mashabiki wake kuwa atakuwa mwaminifu mara hii.

Simba anajulikana kuwahi chumbia wanawake zaidi ya kumi kutoka mataifa mbalimbali kisha kuwatema. 

Amekuwa kwenye uhusiano na Wema Sepetu, Jacqueline Wolper, Tunda Sebastian Irene Uwuoya,Hamisa Mobetto, Rehema Fabian, Jokate Mwegelo, Upendo Mushi,Hawa na Penniel Mungilwa kutoka Bongo, Zari Hassan kutoka Uganda na hivi majuzi amekuwa na Tanasha Donna kutoka Kenya.

Mara hii ameahidi kuwa mwaminifu.