Akothee asherehekea baba watatu wa wanawe watano

Aliwaandikia kuwa anawapenda wote

Muhtasari

•Mwanamuziki huyo wa maika 40 ni mama ya mabinti watatu na wavulana wawili ambao amepata na wanaume watatu tofauti mmoja pekee akiwa Mkenya  huku wawili wakiwa wazungu kutoka Uswidi na Ufaransa.

•Kwenye ujumbe mwingine, mwanamuziki huyo amekashifu wanaume wanaopachika wanawake mimba na kukosa kushirikiana katika male

Akothee na baba za watoto wake
Akothee na baba za watoto wake
Image: Hisani

Mwanamuziki na mwanabiashara maarufu nchini Akothee ametumia siku ya maadhimisho ya kina baba duniani kuwasherehekea baba watatu wa watoto wake.

Mwanamuziki huyo wa maika 40 ni mama ya mabinti watatu na wavulana wawili ambao amepata na wanaume watatu tofauti mmoja pekee akiwa Mkenya  huku wawili wakiwa wazungu kutoka Uswidi na Ufaransa.

Kwenye maadhimisho ya siku ya kina baba duniani, Akothee alitumia mtandao wa Instagram kuwasherehekea  akiwa na ujumbe tofauti kwa kila mmoja wao.

Alianza na mpenzi wake wa hivi karibuni, mzungu kutoka Ufaransa aliyemtambulisha kama Dominique. 

Akothee ana mtoto mmoja wa kiume kwa jina Prince Oyoo na Mfaransa huyo.

Amemsifia Dominique zaidi kwa kumkubali akiwa na watoto wanne tayari na kukubali kuwachukua kama wake.

"Siku ya kufana kwa mwanaume huyu ambaye aliona mama ndani yangu. Baba ya watoto wangu watano, mwanaume wa kipekee niliyepatana naye maishani. Dominique wewe ni kito nadra sana, kuchukua mwanamke aliye na watoto wanne na kuwachukulia kama wako ndicho tunasema ni kitendo cha Mungu" Akothee alimwandikia Dominique.

" Tangu tupatane, tumekuita jina moja tu, 'DAD'. Watoto wangu walienda shule bora zaidi na hujawahi kosa kuhudhuria mkutano wa wazazi. Ulinifungulia milango mpenzi wangu, wewe ni zaidi ya mwokozi.

Wakati wanaume wengine walinichuja kwa sababu ya kuwa na watoto webgi, ulichotaka ni mimi pekee.  Nimeona baba ndani yako na mshauri.

Ulichukua watoto ili niweze kushughulikia taaluma na biashara yangu. Mapenzi yangu yanaendelea kuwa makubwa kila siku na hakuna kilichobadilika. Mungu akulinde" Aliendelea kumwandikia Dominique.

Kwenye chapisho la pili, Akothee alimtakia siku njema ya maadhimisho ya kina baba mpenzi  wake wa kwanza, Jared Otieno, na  ambaye baba ya mabinti wake wanne Vesha Okello, Celly Rue na Prudence Otieno .

"Kila wakati nikitaka kukufuta akilini mwangu  maisha yananikumbusha kuwa singejipachika mimba peke yangu. Shukran kwa malaika watatu ulionipatia. Utabaki kuwa baba ya mabinti wangu watatu. Mungu awe nawe na familia yako. Daddy tunakupenda." Akothee alimwandia Jared.

Kwenye chapisho la mwisho alimsherehekea aliyekuwa mpenzi wake raia wa Uswizi  na ambaye ni baba ya mwanawe wa nne, Prince Ojwang.

""Shukran kwa mwanangu mtanashati na mnyenyekevu. Siku ya kina baba yenye fanaka Papa. Tunakupenda na wewe ni baraka maishani mwangu. Lakini kuwa mpole utulipie holiday wacha kunipa pressure" Akothee alimwandikia baba Ojwan'g.

Kwenye ujumbe mwingine, mwanamuziki huyo amekashifu wanaume wanaopachika wanawake mimba na kukosa kushirikiana katika malezi.

Amesema kuwa ili mwanaume ahitimu kuitwa baba ni sharti awajibike katika maisha yote ya mwanawe.