FAMILIA YA WAJESUS

"Sasa niko tayari kupata binti nawe" Ujumbe wa Milly kwa Kabi tunapoadhimisha siku ya kina baba

Milly alitumia siku ya kusherehekea kina baba kumshukuru mpenzi wake Kabi na ambaye ni baba ya mtoto wake Reign Taji Kabi.

Muhtasari

•Licha ya changamoto zilizokumba ndoa yao wiki kadhaa zilizopita, familia ya Wajesus imeendelea kuonyesha ulimwengu kuwa shinikizo za mitandaoni haziwezi tikisa ndoa iliyo imara.

•"Furahia siku hii, singeomba baba bora  kwa mwanangu zaidi yako. Sasa niko tayari kupata binti na pamoja na wewe" Milly aliandikia Kabi

Milly na Kabi Wajesus
Milly na Kabi Wajesus
Image: Instagram

Licha ya changamoto zilizokumba ndoa yao wiki kadhaa zilizopita, familia ya Wajesus imeendelea kuonyesha ulimwengu kuwa shinikizo za mitandaoni haziwezi tikisa ndoa iliyo imara.

Kabi na mpenzi wake Milly wameendelea mapenzi ndiyo guzo muhimu zaidi katika ndoa na msamaha ni kiungo cha mapenzi.

Milly alitumia siku ya kusherehekea kina baba kumshukuru mpenzi wake Kabi na ambaye ni baba ya mtoto wake Reign Taji Kabi.

"Shukran kwa kuwa baba mzuri kwa mwana wetu. Shukran kwa kufanya kusudi kumwajibikia. Shukran kwa kuomba naye kila usiku kabla ya kulala, jambo hilo linanipea matumaini kuwa Taji Wajesusu atakua kuwa mcha Mungu kama wewe" Milly alimwandikia Kabi kwenye mtandao wa Instagram.

"Furahia siku hii, singeomba baba bora  kwa mwanangu zaidi yako. Sasa niko tayari kupata binti na pamoja na wewe" Aliendelea kusema.

Kabi kwa upande wake alimshukuru mkewe na kumthibitishia kuwa anampenda pamoja na mwanao.

"Shukran sana mpenzi wangu. Nawapenda sana" Kabi aliandika.

Wawili hao walibarikiwa na mtoto mvulana mwaka wa 2019.

Mwezi uliopita, Kabi alishangaza Wakenya baada ya kukiri kuwa ako na binti wa miaka saba na binamu yake.

Hata hivyo, kashfa hiyo haikutikisa ndoa yao kwani wawili hao wameendelea kusherehekeana.