Tuheshimiane!Akothee awaonya wafanyakazi wa KPLC wa Migori

Muhtasari
  • Akothee awaonya wafanyakazi wa KPLC wa Migori
  • Kulingana na Akothee ata baada ya kuwakataza wasiingie ili wajitambulishe walijilaimisha na kuinia nyumbani kwake
Akothee
Image: hisani

Msanii na mwanabiashara Akothee amegadhabishwa na tabia ya baadhi ya wafanyakazi wa KPLC wa kaunti ya Migori baada ya kuingia nyumbani kwake bila idhini.

Kulingana na Akothee ata baada ya kuwakataza wasiingie ili wajitambulishe walijilaimisha na kuinia nyumbani kwake.

Msanii huyo alikumbuka jinsi alilipa bili ya stima ya milioni 1.6 na kuwakumbusha kwamba hajasahau bili hiyo.

Akothee alionya kampuni hiyo kwamba wakati mwingine wafanyakazi wataingia kwake bila idhini, atawachukulia hatua.

"Kenya power Migori, hamnidai chochote,hamna haki yeyote ya kujilazimisha nyumbani kwangu bila idhini

Baadhi ya wafanyakazi wenu hawana heshima, wengine walichukua fursa hiyo kujipigia picha nyumbani kwangu," Aliandika Akothee.

Aliendelea na ujumbe wake na kusihi,kampuni hiyo kuheshimu nyumba za watu, pia aliwapa masharti ambayo wanapaswa kufuata.

"Kusonga mbele vitu viwili 1. Njoo uondoe waya zote zinazopita kwenye kiwanja changu nje ya kiwanja changu ili uweze kuipata wakati wowote unapojisikia.

2.Nitairuhusu tu timu yako na barua rasmi kuja kwenye kiwanja changu na tu na miadi. Walikataa kujitambulisha au hata kutuacha na mawasiliano yao Hakuna mtu anayekuja nyumbani kwangu bila miadi.

3. Tunapokuita kwa jambo la  dharura hata hamjibu kwa hivyo wakala ni wa nini?

4. Wakati mwingine wafanyikazi wako watajilazimisha kuingia kwenye kiwanja changu, nitachukua hatua mikononi mwangu, kwani pia walitishia kukata umeme.

Nilidhani tuliamua katika kulipia tokens, baada ya kuniletea bili ya milioni 1.6nililipa lakini sijawahisahau TUHESHIMIANE 🙏 #KENYAPOWER @kplc_customercare WAAMBIE WAFANYAKAZI WAKO KUHESHIMU NYUMBA ZA WATU."