(+Picha) Simba anguruma Marekani! Diamond akutana na vigogo wa muziki duniani

Diamond pia amefichua kuwa amefanya muziki na Swae Lee wa kikundi cha Rae Sremmund

Muhtasari

•Kupitia picha na video alizopakia kwenye mtandao wa Instagram, Diamond ambaye alienda Marekani kuhudhuria hafla ya kutuza wasanii ya BET Awards 2021 ameonekana akiburudika na wanamuziki wa nyimbo za kufoka waliobobea na kuheshimika kote duniani.

•Kwenye video moja ambayo Diamond alipakia kwenye akaunti yake ya Instagram mapema wiki iliyopita, Busta Rhymes alisikika akimuita Diamond 'Michael Jackson wa Afrika'

Diamond Platnumz na Wiz Khalifa
Diamond Platnumz na Wiz Khalifa
Image: Instagram

Mwanamuziki matata wa nyimbo za Bongo ameendelea kukutana na baadhi ya vigogo wa muziki nchini Marekani.

Kupitia picha na video alizopakia kwenye mtandao wa Instagram, Diamond ambaye alienda Marekani kuhudhuria hafla ya kutuza wasanii ya BET Awards 2021 ameonekana akiburudika na wanamuziki wa nyimbo za kufoka waliobobea na kuheshimika kote duniani.

Kati ya wasanii hao ni ikiwemo Busta Rhymes, OT Genasis, Wiz Khalifa, Akon, Hit Maka na Real Swizz (mtengenaji muziki).

Kwenye video moja ambayo Diamond alipakia kwenye akaunti yake ya Instagram mapema wiki iliyopita, Busta Rhymes alisikika akimuita Diamond 'Michael Jackson wa Afrika'

Inakadiriwa kuwa huenda mwanamuziki huyo ambaye aliibuka wa pili kwenye tuzo la BET kitengo cha International Act anatengeneza muziki na wasanii hao.

Diamond pia amefichua kuwa amefanya muziki na Swae Lee wa kikundi cha Rae Sremmund.

Rhymes ambaye anaheshimika sana kwenye sanaa ya muziki wa kufoka alisema kuwa  Diamond ni mwanamuziki 'hatari