logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mke wangu aliniacha na kusema hawezi lea mtoto ambaye sio wake-Baba yake Ruth Matete afichua haya

Amunga aliongeza kuwa baada ya tukio hilo alichagua kumlea binti yake peke yake.

image
na Radio Jambo

Habari13 July 2021 - 10:41

Muhtasari


  • Abel Amunga afichua sababu yake ya kuamua kumlea Ruth Matete peke yake

Muigizaji wa Kenya Abel Amunga amefunguka jinsi ndoa yake ilivunjika baada ya miaka 5 kwani hawakuweza kupata mtoto.

Amunga ambaye ni baba wa mshindi wa Tusker Project Fame Ruth Matete alikuwa aliachwa na mkewe baada ya miaka mitano katika ndoa.

Akizungumza wakati wa mahojiano na Robert Burale, Amunga alishiriki;

"Binti yangu Ruth alikuwa akiishi na mama yake mzazi na baba wa kambo lakini alikuwa mnyanyasaji sana

Wakati mmoja alimpiga mama ya Ruth juu ya tumbo na alikuwa na ujauzito wa mtoto wao wa tatu

Alipolazwa hospitalini, aliniomba niende kumtoa Ruth kutoka kwa baba yake wa kambo na kukaa naye mpaka wakati atapona

Nilikwenda na kumleta Ruth mahali pangu na kweli waliungana na mama yake wa kambo. Wangeenda kwa matembezi na kufanya vitu pamoja mpaka nikaanza kuwa na wivu wakati fulani.

Walakini baada ya miaka miwili pamoja mke wangu alianza kumtendea vibaya Ruth. Kulikuwa na unyanyasaji wa kihemko, matusi, na hata kimwili. Aliondoka baada ya miaka mitano ya ndoa.

Kutoka kwa kile nilichosikia, Aliwaambia watu alikuwa amechoka kuwa mama wa mtoto ambaye sio wake, alitaka mtoto wake mwenyewe. Tulikuwa tumepitia vipimo na sote tulikuwa sawa. Nilimwambia asubiri Mungu ambariki na mtoto. " Alieleza Amunga.

Amunga aliongeza kuwa baada ya tukio hilo alichagua kumlea binti yake peke yake.

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved