'Ningefurahi sana mwanangu angepata mkenya,'DP Ruto aweka wazi ushauri aliompa mwanawe baada ya kuolewa

Muhtasari
  • DP Ruto aweka wazi ushauri aliompa mwanawe baada ya kuolewa
Naibu William Ruto
Image: Douglas Okiddy

Mwanawe naibu rais William Ruto,June Ruto Alhamisi,Mei,27 2021 ilikuwa siku ya kukumbuka katika maisha yake.

Hii ni baada ya kufunga pingu za maisha na mpenzi wake kutoka Nigeria, hii ni baada ya familia yake kutembela familia ya Ruto.

Ni harusi ambayo iliudhuria na watu mashuhuri, na baadhi ya wanasiasa.

Naibu rais akiwa kwenye mahojiano ya kipekee kwenye Radiojambo siku ya JUmanne alifichua ushauri mkubwa ambao alimpa mwanawe baada ya kupata mume wake.

Huku akiulizwa kama alifurahi kwamba mwanawe aliolewa na mtu kutoka Nigeria, kigogo huyo alisema kwamba angefurahi sana kama mwanawe angeolewa nchini kenya.

USHAURI

"Ushauri mkuu ambao nilimpa mwanangu June ni kuwa anapaswa kufahamu kuwa yuko chini ya mume wake ili ndoa iweze kufaulu

Ningefurahi sana kama mtoto wangu angepata mkenya, lakini hayo yote ni mpango wa Mungu pia chaguo lake

Hapo awali nilikuwa nimesikikia fununu kwamba kulikuwa na Odhiambo lakini sijui alipotelea wapi," Naibu rais alisemah uku akicheka.

Hii hapa video ya mahojiano hayo;