Picha ya siku:Tazama jinsi Omar Lali alipokuwa amepiga luku mahakamani

Muhtasari
  • Tazama jinsi Omar Lali alipokuwa amepiga luku mahakamani
  • Omar, ambaye ndiye mshukiwa mkuu wa mauaji ya Tecra alifika mbele ya mahakama ili kutoa ushahidi wake juu ya tukio hilo lililotokea Mei 2, 2020
Omar Lali

Beach boy ni jina la mtaa la  Omar Lali  aliyopewa na wanamitandao baada ya kufahamika sana baada ya kifo chake Tecra Muigai.

Omar alikuwa katika Mahakama ya Sheria ya Milimani Jumanne kujibu mashtaka juu ya mauaji ya mrithi wa Keroche Tecra Muigai.

Omar, ambaye ndiye mshukiwa mkuu wa mauaji ya Tecra alifika mbele ya mahakama ili kutoa ushahidi wake juu ya tukio hilo lililotokea Mei 2, 2020.

Wakati akionekana mbele ya Hakimu Mkuu Mwandamizi Zainab Abdul, Omar Lali alikuwa amevaa vazi kali.

Omar Lali

Nduguye Omar Lali aliyekuwa mpenzi wa mridhi wa Keroche Bi Tecra Muigai na ambaye ni mshukiwa kwenye mauaji yake ameeleza mahakama kuwa wawili hao walipendana sana na hakuwahi ona wakipigana.

Akitoa ushahidi wake mahakamani siku ya Jumatano, Quswai Lali ambaye ni mfanyakazi katika mkahawa wa Peponi alisema kuwa nduguye alimpigia simu mida ya saa kumi na mbili kasorobo asubuhi na kumuarifu afike kwake.