JE ATAUZA?

'Hii nyumba sio ya kuuzwa!' Omosh aahidi kutouza nyumba mpya aliyojengewa

Kumekuwa na hofu miongoni mwa Wakenya kuwa huenda mwigazaji huyo ambaye amekuwa mhasiriwa wa uraibu wa pombe kwa muda akauza nyumba hiyo ili aweze kukata kiu.

Muhtasari

•Omosh alikabidhiwa nyumba ambayo alijengewa na wadhamini siku ya Jumatano kwenye hafla iliyohudhuriwa na baadhi ya wasanii mashuhuri kama vile Jalango, Fred Omondi, DJ Shiti kati ya wengine.

•Mtangazaji Jalang'o alimkabidhi bango ambalo lilikuwa limeandikwa 'Mali hii si ya kuuzwa' na akampa ushauri kuwa asishawishike kuuza nyumba ile.

Image: HISANI

Hatimaye aliyekuwa mwigizaji wa Tahidi  High Joseph Kinuthia almaarufu kama Omosh anajivunia kuwa mmiliki rasmi wa nyumba.

Omosh alikabidhiwa nyumba ambayo alijengewa na wadhamini siku ya Jumatano kwenye hafla iliyohudhuriwa na baadhi ya wasanii mashuhuri kama vile Jalango, Fred Omondi, DJ Shiti kati ya wengine.

Kumekuwa na hofu miongoni mwa Wakenya kuwa huenda mwigazaji huyo ambaye amekuwa mhasiriwa wa uraibu wa pombe kwa muda akauza nyumba hiyo ili aweze kukata kiu.

Hata hivyo, Omosh aliahidi kuwa hatauza nyumba yake mpya na akatangaza hadharani kuwa nyumba ile si ya kuuzwa.

"Kwetu kuna mila na desturi kuwa huwezi patiwa zawadi ukapatia mtu mwingine kama zawadi ama ukaiuza. Hii ni zawadi na haiwezi uzwa" Omosh alisema.

Mtangazaji Jalang'o alimkabidhi bango ambalo lilikuwa limeandikwa 'Mali hii si ya kuuzwa' na akampa ushauri kuwa asipatwe na tamaa ya  kuuza nyumba ile.

Jalang'o alimwambia Jalang'o aarifu wale ambao walikuwa wakimezea mate nyumba hiyo kuwa si ya kuuzwa.