Niko na vipusa 3 na wote wanataka niwaoe-Barobaro alia

Muhtasari
  • Swali kuu ni je kwanini wanaume wengi hawatosheki na mwanamke mmoja?
  • Mwanamume mmoja nikiwa katika ziara zangu alinisimulia jinsi yuko na vipusa 3 na wote wanataka wamuoe
sad man
sad man

Katika uhusiano wa kimapenzi wengi wamepitia mateso na hata kuumizwa moyo, kuna wale huenda nje ya ndoa na pia wale huwacheza wapenzi wao na wake wengine.

Swali kuu ni je kwanini wanaume wengi hawatosheki na mwanamke mmoja?

Mwanamume mmoja nikiwa katika ziara zangu alinisimulia jinsi yuko na vipusa 3 na wote wanataka wamuoe.

"Nimekuwa nikiwachumbia vipusa watatu, ambapo wanajuana wote niliwatambulisha miezi kadhaa iliyopita

Mmoja wao ana mtoto wangu, lakini nataka kumuoa mmoja wao lakini wote wanataka niwaoe ilhali nataka tu mmoja ambaye ana mtoto wangu sijui nifanye aje na wote wawili hawanielewi

Tumekuwa pamoja kwa miaka 3 sasa nataka kuoa,"

Je mwanamume akiweza kumchumbia mwanamke mmoja anaweza fanya nini au kuna eza tokea nini?