logo

NOW ON AIR

Listen in Live

(Video) Kiki tu! Brown Mauzo apuuzilia mbali madai ya kutengana na Vera Sidika kwa wimbo

Mdahalo ulikuwa umeibuka mitandaoni kuwa wawili hao huenda walikuwa wamekosana licha ya wao kutesa wanamitandao kweli kwa picha na jumbe kochokocho za mapenzi kwa kipindi kirefu.

image
na Radio Jambo

Habari16 July 2021 - 08:24

Muhtasari


•Mdahalo ulikuwa umeibuka mitandaoni kuwa wawili hao huenda walikuwa wamekosana licha ya wao kutesa wanamitandao kweli kwa picha na jumbe kochokocho za mapenzi kwa kipindi kirefu.

•Kweli mwanamuziki huyo kahutubia Wakenya ila ni kwa wimbo ambao unazungumzia safari ya ujauzito wa mkewe.

Masalale! Kumbe hatua ya mwanamuziki Brown Mauzo kukosa kuonekana kwenye sherehe ya kufichua jinsia ya mtoto aliyebeba mpenziwe Vera Sidika ilikuwa kiki tu!

Hii imebainika wazi baada ya mwanamuziki huyo toka Pwani kupakia kibao alichomtungia Vera kwenye mtandao wa YouTube siku kadhaa baada ya sherehe hio kufanyika.

Mdahalo ulikuwa umeibuka mitandaoni kuwa wawili hao huenda walikuwa wamekosana licha ya wao kutesa wanamitandao kweli kwa picha na jumbe kochokocho za mapenzi kwa kipindi kirefu.

Siku ya Alhamisi Mauzo alitangaza kupitia mtandao wa Instagram kuwa angehutubia Wakenya kuhusiana na tukio lake kukosa kwenye sherehe hiyo mnamo Ijumaa(leo0

Kweli mwanamuziki huyo kahutubia Wakenya ila ni kwa wimbo ambao unazungumzia safari ya ujauzito wa mkewe.

Tazama hapa;

Awali kabla ya kupakiwa kwa wimbo huo, Vera alikuwa ameandika ujumbe akiwasihi wanaume  kutofikiria 'kuhutubia wananchi' baada ya mambo kuenda mrama kwani  hakuna aliyefurahia utamu wa tendo la ndoa pamoja nao" Vera aliandika..

"Wanaume, ulipokuwa unamvua nguo, mlikuwa peke yenu. Hakuna ambaye alikuwa nanyi wakati mlikuwa mnafurahia utamu wa tendo la ndoa. Kwa hivyo usifikirie kuhutubia wananchi baada ya mambo kuenda mrama

Katikati mwa mwezi uliopita, mwanasoshalaiti huyo alitangaza wazi kuwa alikuwa akitarajia mtoto na mpenzi wake Brown Mauzo.

Matokeo ya vipimo yaliyotangazwa usiku wa Jumamosi yalithibitisha kuwa msanii huyo amebeba mtoto wa kike.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved