Eric Omondi atengeneza Sh3.6M kwa kutumbuiza mashabiki 46,000 Tanzania baada ya kuitwa maskini

Alisema kuwa kazi ya Ezekiel Mutua ni kuketi tu, kupaka nywele yake rangi nyeusi, kubadhirisha pesa za umma ili kujisaidia mwenyewe na akadai kuwa hana haki ya kutusi waliomwajiri.

Muhtasari

•Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Eric ambaye alitumbuiza mashabiki  akiwa pekee yake alifichua kuwa tamasha hiyo ilimletea faida ya shilingi milioni 3.6. 

•Eric pia alitumia fursa hiyo kumkosoa bosi wa KFCB Ezekiel Mutua kwa kile alisema ni kumdhalilisha na kumpatia hadi Jumatatu kumwomba msamaha.

Image: INSTAGRAM

Mcheshi tajika kutoka Kenya Eric Omondi anajivunia kuvutia halaiki kubwa ya zaidi ya mashabiki 45,000 katika uwanja wa Uhuru nchini Tanzania.

Kulingana na mcheshi huyo, tamasha ya hivi karibuni ambayo alifanya jijini Dar es Salaam ilihudhuriwa na mashabiki 46000.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Eric ambaye alitumbuiza mashabiki  akiwa pekee yake alifichua kuwa tamasha hiyo ilimletea faida ya shilingi milioni 3.6. 

"Nilijaza uwanja na watu 46,000 katika nchi ya kigeni  na nikatengeneza faida ya Ksh 3.6M." Eric alisema.

Eric pia alitumia fursa hiyo kumkosoa bosi wa KFCB Ezekiel Mutua kwa kile alisema ni kumdhalilisha na kumpatia hadi Jumatatu kumwomba msamaha.

Alisema kuwa kazi ya Mutua  ni kuketi tu, kupaka nywele yake rangi nyeusi, kubadhirisha pesa za umma ili kujisaidia mwenyewe na akadai kuwa  hana haki ya kutusi waliomwajiri.

"Ambieni yule jamaa mwizi mzee kuwa CEO aliyeajiriwa hawezi bishana na rais.. Kazi yake ni kuketi na kupaka nywele yake rangi nyeusi, kubadhirisha pesa za umma ili kujisaidia mwenyewe na anapata ujasiri wa kutusi walimuajiri(Wasanii). Ako na masaa 14 kuomba msamaha" Alisema Eric.

Wasanii wengine kama vile Khaligraph Jones wamejitokeza kumuunga Eric mkono na kumkosoa bosi wa KFCB.

Mcheshi huyo kwa sasa yuko Tanzania kwa ziara ya kikazi.