logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Siwezi rudiana naye,' Aliyekuwa mkewe Harmonize amjibu baada ya kumuomba msamaha

Walienda kwenye hafla pamoja, na pia kuwafanya mashabiki kuwaona wao ni wanandoa kamili.

image
na Radio Jambo

Habari21 July 2021 - 11:16

Muhtasari


  • Aliyekuwa mkewe Harmonize amjibu baada ya kumuomba msamaha
harmonize.696x524

Mwimbaji wa Tanzania Harmonize aliwaacha mashabiki wake kwenye bumbuwazi jana usiku baada ya kuomba msamaha hadharani kwa mkewe wa zamani Sarah kwenye akaunti yake ya Instagram.

Wawili hao walikuwa pamoja kwa miaka minne, uhusiano wao ulikuwa wa kupendeza zaidi kati ya wanandoa wengine mashuhuri.

Walienda kwenye hafla pamoja, na pia kuwafanya mashabiki kuwaona wao ni wanandoa kamili.

Baada ya uhusiano wa miaka minne, Sarah alifahamu juu ya mtoto wa siri wa Harmonize ambaye alibarikiwa na mwanamke mwingine bado akiwa kwenye uhusiano naye.

Ingawa alimtambulisha binti yake kwa umma na baadaye akaomba msamaha kwa kumficha Sarah, hakusikia yoyotebali waliachana baada ya hayo.

"Samahani ndilo neno pekee naweza tumia kwa mwanamke huyu mrembo πŸ‘© Alienipatia Miaka (4) Ya maisha Yake Nami Nikampatia (4) Yangu Tulipitia Mengi Ila itoshe Kusema Nilizingua Sanaa ..!!! Mpaka Mungu Alipoamua Kuniletea Mtoto Wangu wa Kwanza @zuuh_konde Na Ndo Ikawa Mwisho Wa Safari Yetu Ya Pamoja. Naaam KUTELEZA KUNATOKEA Naa Muungwana Huomba Radhi πŸ™ ila Ningeonekana Mjinga Zaidi Ningeendelea Kumficha Mtoto Wangu" Alisema Harmonize.

Baada ya Sarah uona msamha wa Harmonize alimjibu na kusema kwamba hawezi rudiana naye.

"Hata akiomba msamaha siwezi rudiana naye, ndo ni ukweli alifanya vibaya, tumepeana block kila mahali hatuzungumzi naye," Sarah Alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoΒ© Radio Jambo 2024. All rights reserved