Akothee ambubujikia sifa baby daddy Mfaransa kwa kulea wanawe baada ya kuwalaki nchini

Mwanamuziki huyo alisema kuwa anawaheshimu sana 'baby daddies' wake ila anamheshimu zaidi babake Oyoo kwani anafanya kusaidiana katika ulezi kuwa rahisi.

Muhtasari

•Wawili hao walitua katika uwanja wa ndege wa JKIA usiku wakiandamana na baba mzazi wa Oyoo ajulikanaye kama Dominic ambaye wanaishi naye.

•Akitangaza kuwasili kwao kwenye mtandao wa Instagram, mama huyo wa watoto watano alimshukuru sana baba wa kitinda mimba  wake kwa kukubali ombi lake kuja Kenya kuwaona wazazi wake.

Papa Oyoo na Akothee
Papa Oyoo na Akothee
Image: INSTAGRAM

Akothee almaarufu kama Madam Boss ni mama mwenye furaha baada ya kuwapokea wanawe wawili Prince Ojwang na Prince Oyoo nchini kutoka Ufaransa.

Wawili hao walitua katika uwanja wa ndege wa JKIA usiku wakiandamana na baba mzazi wa Oyoo ajulikanaye kama Dominic na ambaye wanaishi naye.

Akothee ambaye alikuwa ameandamana na binti wake wawili Rue Baby na Vesha Okello kuwalaki alionekana mwenye bashasha si haba kuwaona wanawe baada ya kipindi kirefu.

Akitangaza kuwasili kwao kupitia mtandao wa Instagram, mama huyo wa watoto watano alimshukuru sana baba wa kitinda mimba  wake kwa kukubali ombi lake kuja Kenya kuwaona wazazi wake.

Akothee alisema kuwa atampeleka kijijini kwao Rongo ili wazazi wake wakamshukuru kwa kukubali kumsaidia kulea watoto.

"Shukran kwa kuheshimu ombi langu kuja kuonababangu kwani amekuwa akikuulizia. Kesho nakupela kwetu Rongo, kule nilikozaliwa wazazi wangu wakushukuru kwa kuwalea watoto wetu" Akothee alisema.

Mwanamuziki huyo alisema kuwa anawaheshimu sana 'baby daddies' wake ila anamheshimu zaidi babake Oyoo  kwani anafanya kusaidiana katika ulezi kuwa rahisi.