Hongera! Larry Madowo apandishwa cheo CNN

Madowo, 34, aliweka wazi kuwa amehamia jijini Atlanta, Georgia ambako atakuwa akifanyia kazi.

Muhtasari

•Miezi miwili tu baada ya mzaliwa huyo wa Siaya, Kenya kujiunga na CNN kama mwandishi wa habari anayeripotia Nairobi, sasa amepandishwa cheo na atakuwa mwandishi wa habari wa kimataifa katika kampuni hiyo.

•Madowo alianza taaluma yake ya wandishi wa habari katika runinga ya KTN kabla ya kujiunga na NTV. Aliwahi kufanya kazi katika stesheni ya CNBC Africa nchini Afrika Kusini.

madowo1
madowo1

Nyota ya mwanahabari Larry Madowo imeendelea kung'aa kila uchao huku akiendelea kupata mafanikio makubwa kwenye taaluma ya uandishi wa habari.

Miezi miwili tu baada ya mzaliwa huyo wa Siaya, Kenya kujiunga na CNN kama mwandishi wa habari anayeripotia Nairobi, sasa amepandishwa cheo na atakuwa mwandishi wa habari wa kimataifa katika kampuni hiyo.

Madowo, 34, alitangaza mafanikio hayo kupitia mtandao wa Facebook na kuweka wazi kuwa amehamia jijini Atlanta, Georgia ambako atakuwa akifanyia kazi.

Kabla ya kujiunga na CNN mwezi Mei mwaka huu Madowo alikuwa ameajiriwa kwa kampuni ingine ya kimataifa BBC kama mwandishi wa habari maeneo ya Marekani Kaskizini.

Madowo alianza taaluma yake ya wandishi wa habari katika runinga ya KTN kabla ya kujiunga na NTV. Aliwahi kufanya kazi katika stesheni ya CNBC Africa nchini Afrika Kusini.