'Naomba Mungu alinde umoja wao,'Ujumbe wake Bahati kwa Vera Sidika na Brown Mauzo

Muhtasari
  • Bahati awapongeza Vera sidika na Brown Mauzo
  • Mwanasosholaiti Vera Sidika na mumewe Brown Mauzo wanatarajia mtoto wao wa kwanza,tanu kufunga pingu zao za maisha
  • Vera aliweka wazi kwamba alibeba ujauzito wa mpenzi wake Februari mwaka huu siku ya wapendanao
Bahati
Bahati
Image: Instagram

Mwanasosholaiti Vera Sidika na mumewe Brown Mauzo wanatarajia mtoto wao wa kwanza,tanu kufunga pingu zao za maisha.

Vera aliweka wazi kwamba alibeba ujauzito wa mpenzi wake Februari mwaka huu siku ya wapendanao.

Mapema mwezi wa Julai mwanasosholaiti huyo alifichua jinsia ya mtoto wake.

Mashabiki, na watu tofauti wamekuwa wakiwatumia wawili hao jumbe za kuwapongeza, kwa hatua yao.

Vera hajaweza kuficha furaha yake anapotarajia kuwa mama, kwa mara ya kwanza,Pia amekuwa akimpongeza Mauzo kwa kubadili maisha yake.

Msanii Bahati kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram, amewapongeza wawili hao na hata kumuomba Mungu abariki na kulinda umoja wao.

"Mapenzi ni kitu mzuri hasa unapopata mtu sahihi ndugu yangu @brown Mauzo yuko kwenye upendo

KIle  ninacho omba Mungu ni alinde umoja wao, na awajaze na furaha , maishani mwao yote," Aliandika Bahati.