R. Kelly ashtumiwa kumdhulumu kimapenzi mvulana wa miaka 17

Mashtaka hayo yanahusisha wanawake na wasichana sita ambao hawajatajwa majina.

Muhtasari

•Mshindi huyo wa tuzo ya Grammy, ambaye jina lake halisi ni Robert Kelly, anatarajiwa kushtakiwa New York mwezi ujao kwa mashtaka yakiwemo unyanyasaji wa kingono wa watoto,kuchukua picha mbaya za watoto, udanganyifu na uzuiaji wa haki.

•Wao ni pamoja na mvulana wa miaka 17 na mwanamuziki mtarajiwa , ambaye Kelly anadaiwa alikutana naye katika McDonald's na kisha akamwalika kwenye studio zake huko Chicago.

R.Kelly
R.Kelly
Image: HISANI

Mwanamuziki wa Marekani wa R&B R. Kelly amekabiliwa na shutuma mpya za kumdhulumu kimapenzi mvulana mwenye umri wa miaka 17 .

Waendesha mashtaka wanadai mwimbaji huyo alimnyanyasa kijana huyo baada ya kukutana naye huko Chicago katika mkahawa wa McDonald's mnamo 2006.

Wanataka ushahidi wa dhulma hizo na uhalifu mwingine unaodaiwa kutekelezwa naye ambao hakushtakiwa ujumuishwe katika kesi ya Kelly mnamo Agosti.Kelly anakanusha kumnyanyasa mtu yeyote, na mawakili wake hawajajibu madai haya ya hivi karibuni.

Mshindi huyo wa tuzo ya Grammy, ambaye jina lake halisi ni Robert Kelly, anatarajiwa kushtakiwa New York mwezi ujao kwa mashtaka yakiwemo unyanyasaji wa kingono wa watoto,kuchukua picha mbaya za watoto, udanganyifu na uzuiaji wa haki.

Mashtaka hayo yanahusisha wanawake na wasichana sita ambao hawajatajwa majina.

Sasa, waendesha mashtaka pia wangependa mawakili kusikia juu ya zaidi ya watu wengine kadhaa ambao wanasema Kelly aliwanyanyaswa, kutishiwa au kutendewa vibaya.

Wao ni pamoja na mvulana wa miaka 17 na mwanamuziki mtarajiwa , ambaye Kelly anadaiwa alikutana naye katika McDonald's na kisha akamwalika kwenye studio zake huko Chicago.