King Alami amuomba mpenzi wake Notiflow msamaha hadharani

Muhtasari
  • King Alami amuomba mpenzi wake Notiflow msamaha hadharani
King Alami na Notiflow
Image: Instagram

Wiki chache zilizopita uhusiano wa kimapenzi wa  msanii Notiflow na mpenzi wake King Alami ulikwisha baada ya wawili hao kutengana.

Kulingana na Notiflow sababu yao ya kuacha ni kwa maana walichapana, huku akidai kwamba karibu aliyekuwa mpenzi wake amuue.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram wa King Alami alimuomba Notiflow msamaha kwa yote ambayo alimtendea.

Alami alikubali makosa yake na kusema kwamba alikuwa mkali kwa mpenzi wake.

"Nataka kuomba msamaha hadharani kwa mpenzi wangu @Notiflow, jambo la kwanza kwa kuwa mkali kwake, kumuumiza kimwili na kihemko

Jambo la pili kwa kumnyanyasa na kumpigia kelele, la tatu nilikuwa nataka kuweka haya hapa ili kutupilia mbali jinsi watu walichukulia mambo," Aliandika Alami.

Pia Notiflow aliweka wazi kwamba hawezi mrudia Alami kwa sababu ya tofauti zao na karibu amtoe uhai.