Hamna mtu aliyekuekea bunduki kichwani mwako,'Vera awaonya wanaokejeli safari yake ya ujauzito

Muhtasari
  • Vera awaonya wanaokejeli safari yake ya ujauzito
  • Kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii ya instagram aliwaambia wote ambao wamechoka kuona hadi picha wake wamwambie kwani atawapa block
Image: INSTAGRAM//VERA SIDIKA

Mwanasoshalaiti Vera Sidika anaonekana kuchoshwa na wanamitandao ambao wanakejeli safari ya ujauzito wake.

Kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii ya instagram aliwaambia wote ambao wamechoka kuona hadi picha wake wamwambie kwani atawapa block.

PIa aliweka wazi kwamba hamna mtu ambaye aliwalazimisha au kuweka bunduki vichwani mwao ili watazame picha zake na kushuhudia safari ya ujauzito wake.

"Ikiwa umechoka na picha zangu za ujauzito, safari na uzoefu tafadhali nitumie DM. Nataka kufanya maisha yako kuwa rahisi.

Nampa block kila mtu ambaye amechoka kuwa kwenye ukurasa wangu, kumbuka hakuna mtu aliyeweka bunduki kichwani mwako na kukulazimisha hapa. Ninafuta uzembe wote kwa njia bora zaidi. " Aliandika Vera.

Mwanasosholaiti na mwanabiashara Vera Sidika kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alifichua kwamba hataki kuzaa au kijifungua kawaida bali kupitia upasuaji.

Vera alisema kwamba tangu ajue maana ya kujifungua hajawahi tamani kujifungua kwa kawaida kwani anafahamu kuna maumivu tofauti.

"Tangu nilipofikiria kuwa na watoto katika maisha yangu ya watu wazima, nilijiambia nitafanya hivyo ikiwa sio lazima nipate kazi. Kwa hivyo nimekuwa timu CS milele (imepangwa). Sitaki kuhisi inchi ya maumivu ya leba. Kuwa na wigi yangu na vipodozi kwenye mkondo wakati wa kujifungua.