logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Katika maisha kitu cha maana ni amani ya akili-Ushauri wake Betty Bayo kwa mashabiki

Kulingana na msanii huyo kuna uamuzi watu huchukua unaumiza,

image
na Radio Jambo

Habari05 August 2021 - 12:15

Muhtasari


  • Kulingana na msanii huyo kuna uamuzi watu huchukua unaumiza, bali mtu huyo anahitaji amani ya akili yake

Msanii wa nyimbo za injili Bettty Bayo kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amewashauri mashabiki wake kwa nini kuwa na amani ya akili ni muhimu.

Kulingana na msanii huyo kuna uamuzi watu huchukua unaumiza, bali mtu huyo anahitaji amani ya akili yake.

Huu hapa ushauri wake

"Kwanini mtu huwa anaacha nyumba ambayo imejengwa vizuri na kuto beba chochote, na kuenda kukodisha nyumba ya chumba kimoja na kulala chini?

Inaitwa amani ya akili kwanini mtu huacha kazi ambayo anapokea mshahra mzuri, na kuanzisha kibanda yake? inaitwa amani ya akili

Kwanini mtu huacha ndoa ya zaidi ya miaka 20 na kuanza kuishi pekeyake na kujitegemea? inaitwa amani ya akili

Katika maisha kile kina maana ni amani ndogo ya akili,watu wengi hufanya uamuzi katika maisha yao na watu kuona ni uamuzi wa kijinga na usio na busara, lakini ukiwa katika hali yao utawaelewa vyema'Amani ya akili ni kila kitu," Aliandika Betty.

Je una amani ya akili, ni kitu cha maana ambacho wananchi wengi wanahitaji kwa sasa hasa wakati huu visa vya mauaji vimezidi kurekodiwa nchini.

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved