Zari amwandikia kifungua mimba wake ujumbe wa kipekee anaposherehekea siku yake ya kuzaliwa

Muhtasari
  • Zari amwandikia kifungua mimba wake ujumbe wa kipekee anaposherehekea siku yake ya kuzaliwa

Zari Hassan ni  mjasiriamali na mama wa watoto watano wazuri na wenye urembo wa kipekee,Zari anaishi Afrika Kusini na familia yake.

Wanawe wa kwanza watatu, alibarikiwa na mumewe marehemu Ivan Ssemwanga na  wawili ni kutoka kwa mwanamuziki wa Kitanzania na mwandishi wa nyimbo Diamond platinumz.

Baada ya sherehe ya binti yake, Zari ameamua kumsherehekea mtoto wake ambaye sasa ni mtu mzima kwani leo anafikisha miaka 18.

Inasemekana anafanana kabisa na marehemu baba yake na ndiye aliyepewa kurithi utajiri wake mwingi.

Pinto anajulikana kuwa na nidhamu sana na mchapakazi na hii ndio kila mama angependa kwa mwanawe.

Miezi michache iliyopita, Zari alikuwa ameahidi kumpa gari akiwa na umri wa miaka 18 na sasa tunasubiri kuona ikiwa ahadi hiyo itatimizwa.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Zari alikuwa na haya ya kumwambia mwanawe;

"Nisaidie kumtakia mtoto wangu heri ya miaka 18 ya kuzaliwa. Hewa, ni Mungu tu ndiye anajua jinsi nilivyoomba kuwa hapa siku hii

Kuwa mtoto wangu wa kwanza nilitumia siku zangu nyingi kukutazama nikijiuliza utakuwaje. Na kwa neema ya Mungu hapa tuko. Tumebarikiwa sana 🙌. Heri ya siku ya kuzaliwa na kuombea miaka mingi zaidi ya maisha iliyo mbele. Nakupenda @ pinto.tlale," Aliansika Zari.