Betty Kyallo azungumza baada ya kuwa kwenye orodha ya waliosakwa sana kwenye Google katika kipindi cha miaka 15 iliyopita

Muhtasari
  • Betty Kyallo azungumza baada ya kuwa namba 7 katika utafutaji wa google kwa miaka 15 iliyopita
  • Hizi ni baadhi ya utafutaji ambao Wakenya wamekuwa wakitafuta, kwa miaka 15 iliyopita
  • Google ilitoa data siku ya Jumatano kusherehekea maadhimisho ya miaka 15
89602643_673041820116574_6405692330918304730_n
89602643_673041820116574_6405692330918304730_n

Jinsi ya kufanya mapenzi, mwanasheria Miguna Miguna, Kenya Power na Ligi Kuu ya Uingereza.

Hizi ni baadhi ya utafutaji ambao Wakenya wamekuwa wakitafuta, kwa miaka 15 iliyopita.

Google ilitoa data siku ya Jumatano kusherehekea maadhimisho ya miaka 15.

Katika orodha hiyo mwanahabari, na mwanabiashara Betty Kyallo aliibuka nambari ya saba, katika utafutaji wa google.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instgram Betty alisema kwamba kuwa nambari 7 sio rahisi kwani amepitia magumu katika miaka michache iliyopita.

"Hii ilitokea leo. Ninathamini kwa uaminifu maslahi. Nambari ya wema 7 'ni kweli nilikuwa nimepitia milima na mabonde katika maisha na baada ya kuanza kazi yangu ya uhanahabari nikiwa kijana nimekwenda kwa njia nyingi katika jicho la umma ambayo si rahisi

Kwa kweli ni ngumu sana. Ni kama kuishi ujana wako pamoja na maisha ya watu wazima na kila mtu akiangalia

Nini kinanipa shukrani nyingi juu ya yote haya ni kwamba nimewaongoza watu wengi njiani na safari yangu kupitia maisha," Alisema Betty.

Aliendelea na kunakili ujumbe wake na usema kuwa;

"Kwamba unaweza kuwa sahihi juu yako mwenyewe na unaweza kujipenda bila msamaha Kwa njia hii yote niliyojifunza jinsi ya kurudi nyumbani kwangu

Na ndio maana ni muhimu sana na yenye nguvu. Unapaswa kufanya hivyo pia. Ninaomba kwamba tutaendelea kujifunza pamoja kwa muda mrefu kama Mungu anatupa uzima. Asante! Shukrani kwa @Google kwa hili,"Betty aliandika.

Wanamitandao na mashabiki walichukua fursa hiyo na kumpongeza Betty.

Miongoni mwa wakenya wengine ambao walikuwa katika orodha hiyo ni pamoja na raia Uhuru Kenyatta,naibu rais William Ruto, babu Owino,Miguna,raila Odinga,kanze dena,bob collymore,mike sonko,miongoni mwa wengine.