'Nithamini nikiwa hai,'Zari Hassan akashifu unafiki wa watu baada ya kifo cha mpendwa wao

Muhtasari
  • Zari Hassan akashifu unafiki wa watu baada ya kifo cha mpendwa wao
Zari Hassan
Image: Maktaba

Baada ya kifo cha mpendwa au mtu mashuhuri, tumewaona wengi wakiwashukuru na kuwapa sifa baada ya kifo chao.

Hamna mtu ambaye amekuwa akisifiwa kwa mabaya bali wamekuwa wakimlimbikizia sifa na mambo mema.

Swali ni, Je! Kwanini hauthamini mtu wakati anaweza kuelezea ukweli wako?

Zari ameweka wazi kupitia akaunti yake ya Instagram kwamba watu waachane na unafiki wa kuwasifu wasio na uhai.

Alisisitiza kuwa watu wanahitaji kupenda na kuthamini wakati ambapo anaweza kuhisi haya yote.

Huu hapa ujumbe wake

"Inasikitisha lakini hii ndio jinsi watu wanavyokukumbuka wakati umeenda. Ujumbe wote mzuri wa hii na ile. Smh ninyi wanafiki 🤣. Nithamini wakati nipo hapa, nitumie maua wakati bado ninaweza kunukia. Wapende watu wakati bado unaweza," Zari Aliandiika.

Hizi hapa baadhi ya hisia za mashabiki;

sumiaffolter: I love and appreciate you. Also sending roses right now ❤️

dida3558: Wooh mungu akulinde n husda zao mbaya zigeuke kuwa baraka kwako!❤️❤️❤️

daima451: That's true my Boss❤️❤️❤️

evabril_001: You're saying the pure truth mama tiffah