Kabi wa Jesus aanza ujenzi wa nyumba yao kama 'birthday surprise' kwa mpenzi wake Milly

Mtumbuizaji Kabi aliamua kushangaza mpenziwe akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa kumfichulia kuhusu hatua yake ya kuanza kujengea nyumba ya familia.

Muhtasari

•Peter Kabi almaarufu kama Kabi wa Jesus na mpenzi wake Milly wa Jesus wameanza ujenzi wa nyumba yao mahali pasipotambulishwa.

•Walipokuwa pale shambani Kabi alimfichulia Milly kuwa alikuwa amefanya maamuzi kuanza kujenga nyumba yao kama zawadi yake ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa.

Image: INSTAGRAM//KABI WA JESUS

Peter Kabi almaarufu kama Kabi wa Jesus na mpenzi wake Milly wa Jesus wameanza ujenzi wa nyumba yao mahali pasipotambulishwa.

Mtumbuizaji Kabi aliamua kushangaza mpenziwe akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa kumfichulia kuhusu hatua yake ya kuanza kujengea nyumba ya familia.

Wanavlogu hao walijulisha mashabiki wao kupitia video ambayo walipakia katika mtandao wa YouTube siku ya Ijumaa.

Kwenye video hiyo, Kabi alimfunga macho Milly na kumpeleka hadi mahali walinunua shamba Milly akiadhimisha kufikisha miaka 27 mwaka uliopita.

Walipokuwa pale shambani Kabi alimfichulia Milly kuwa alikuwa amefanya maamuzi kuanza kujenga nyumba yao kama zawadi yake ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa.

"Najua kuna vitu mingi sana ulikuwa ukitaka lakini hii hapa hukuwa unatarajia. Nina raha sana kwamba hatimaye tumeanza kufanya jambo hili.. mpenzi wangu kama nilivyoahidi mwaka uliopita, nimeamua kwamba ni wakati tuanze kujenga" Kabi alimwambia Milly.

Hafla ya kuzindua ujenzi wa nyumba ya familia ya Wa Jesus  ilihudhuriwa na marafiki wao wachache.

Milly alimshukuru Kabi kupitia ukurusa wake wa Intagram na kumwambia kuwa alikuwa ameridhishwa  na hatua ile.

"Hii ndiyo 'surprise' nzuri sana nishawahi kupata. Asante sana mfalme wangu kwa kufikiria zaidi na kuwa na mawazo ya kipekee. Hata mimi sikutarajia hayo. Mimi ni msichana mwenye raha" Milly alimwandikia Kabi.

Kabi alisema kuwa mawe itakayotumika kujenga nyumba hiyo ingeanza kuwasili wiki hii.

Milly aliadhimisha kufikisha miaka 28 siku ya Jumanne wiki hii. 

Mwaka uliopita Kabi alinunua shamba kama zawadi ya siku ya kuzaliwa kwa mpenzi wake.