Je ni kweli ndoa ya dadake Diamond, Queen Darleen imevunjika? Azungumia madai kuwa ameachwa

Darleen ambaye ni dada ya staa mkubwa wa Bongo Diamond Platnumz ameashiria dalili kuwa huenda ni kweli ndoa yake ya miaka miwili imevunjika

Muhtasari

•Akiwa kwenye mahojiano na mwanahabari mmoja nchini Tanzania, Darleen amesema kuwa ndoa sio kitu cha aibu na vilevile kuachwa sio aibu pia.

•Uvumi ulianza kuenea Bongo kwamba mama huyo wa watoto wawili ameachwa haswa baada yake kuacha kupakia picha za mumewe kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

•Darleen amesema kuwa ataendelea kupatia mtoto wake wa miezi tisa malezi bora mwenyewe na kumlinda kutokana na mahangaiko hadi atimize mmoja ndipo arudi katika kazi zake.

Image: INSTAGRAM//QUEEN DARLEEN

Mwadada mwanamuziki mashuhuri kutoka Bongo Mwanajuma Abdul Juma almaarufu kama Queen Darleen amefunguka kuhusu ndoa yake ya na kuzungumzia madai kuwa ametengana na mumewe Isihaka Mtoro.

Darleen ambaye ni dada ya  staa mkubwa  wa Bongo  Diamond Platnumz ameashiria  dalili kuwa huenda ni kweli ndoa yake ya miaka miwili imevunjika.

Akiwa kwenye mahojiano na mwanahabari mmoja nchini Tanzania, Darleen amesema kuwa ndoa sio kitu cha aibu na vilevile kuachwa sio aibu pia.

"Siko tayari kuzungumzia hizo vitu. Kama nimeachika basi riziki  yangu imeshakwisha huko kwa hivyo maisha yangu kwingine yanaendelea. Hakuna chochote kinachoniumiza mimi ama kunizuia. Kwanza kuolewa sio aibu, kuachika pia sio aibu. Kama mahali umechoka una uwezo wa kuamua wewe mwenyewe. Siwezi kujifaidisha kusema eti fulani atanichukilia aje nani atasemaje ikiwa maumivu yangu wao hawayajui. Kwa hivyo kuachika kwangu mimi, hayo ni maisha yangu, kutoachika pia ni maisha yangu" Queen Darleen alisema.

Uvumi ulianza kuenea Bongo kwamba mama huyo wa watoto wawili ameachwa haswa baada yake kuacha kupakia picha za mumewe kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Kwa muda wanandoa hao walitangaza mapenzi yao yaliyoonekana matamu kweli kwenye mitandao ya kijamii.

"Nilishaamua na nikasema kabisa kwamba sitakuja  kumpost tena mtu  yeyote ambaye hana uhusika na mimi kimahusiano... mimi siwezi kumakaza mtu yeyote kuongea... niliamua tu nikasema kama vile tu nilimtambulisha kwa jamii na vile vile nikasema kwamba siwezi kumpost tena" Msanii huyo alisema.

Licha ya hayo Darleen amesema kuwa ataendelea kupata watoto hata kama hatakuwa kwenye mahusiano ya ndoa.

"Mimi nitazaa mpaka dunia itakaposema top unatakiwa sasa kurudi. Kuzaa nitazaa kwa sababu kizazi ninacho. " Alisema Darleen

Darleen amesema kuwa ataendelea kupatia mtoto wake wa miezi tisa malezi bora mwenyewe na kumlinda kutokana na mahangaiko hadi atimize mmoja ndipo arudi katika kazi zake.

Msanii huyo pia alisema kuwa hana ugomvi na dadake Esma Platnumz ila ni kawaida yao kukwaruzana mara kwa mara.