'Unajua jinsi nakupenda,'Diamond asherehekea siku ya kuzaliwa na ndugu yake Romy Jons

Muhtasari
  • Diamond asherehekea siku ya kuzaliwa na ndugu yake Romy Jons
Image: WASAFI

Bila shaka msanii na staa wa bongo Diamond Platnumz ni mfalme wa nyimbo zabongo flava Afrika mashariki.

Bali na kazi yake msanii huyo anapenda familia yake, na kuitambua.

Kwa muda sasa Diamond amekuwa akiongoza, na kuwa na wafuasi wengi kwenye vibao vyake vya hivi juzi.

Je kuna msanii ambaye anaweza vunja rekodi ya msanii huyo?Pia ni mkurugenzi mkuu wa lebo ya muziki ya Wasafi.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alipakia picha ya zamani yake na ndugu yake Rommy huku akimtakia siku njema akisherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Kutokana na picha hizo ni wazi kwamba wawili hao walikuwa na uhusiano wa karibu sana nyakati zao za utotoni.

Pia alimwambia kwamba anafahamu jinsi anampenda.

Huu hapa ujumbe wake;

"Unajua jinsi ninavyokupenda ndugu yangu @romyjons," Aliandika Diamond.

Hizi hapa baadhi ya jumbe za mashabiki

_esmaplatnumz: WADOGO ZANGU 👩‍👦‍👦

iam_akujumbosso: @diamondplatnumz namwona nasib jr😂

wakuzoza: wa2 wanatoka mbali asee simba

vannnesamdeefunpage: mapacha toka zamani

swerry_bby: Du ulikua mtundu inaonekan😂😂😂

evans_wangunda: Happy birthday brothers 🔥🔥🔥❤️❤️

victor_good_son: So mchezo mbali Sana