(+Video) Je ilikuwa kiki? Nadia Mukami na Arrow Bwoy washirikiana kwa wimbo baada ya kutangaza wanachumbiana

Kwenye wimbo huo wawili hao wanasikika kusifiana huku wakifungua roho zao kuhusu mapenzi makubwa ambayo kila mmoja anayo kwa mwenzake.

Muhtasari

•Wanandoa wapya mjini wasanii Arrow Bwoy na Nadia Mukami wameshirikiana kutoa kibao moto sana  'Raha' 

•Hata hivyo kuna wasiwasi kuwa huenda tangazo lao kuwa wanachumbiana lilikuwa kiki tu kwani sio mara ya kwanza Nadia kutambulisha mwanaume kama mpenzi wake kisha akatoa wimbo

Image: INSTAGRAM//NADIA MUKAMI

Wanandoa wapya mjini wasanii Arrow Bwoy na Nadia Mukami wameshirikiana kutoa kibao moto sana  'Raha' 

Kulingana na wasanii hao, wimbo huo ambao walipakia kwenye mtandao wa YouTube asubuhi ya Jumatatu kinazungumzia safari yao ya mapenzi.

Kwenye wimbo huo wawili hao wanasikika kusifiana huku wakifungua roho zao kuhusu mapenzi makubwa ambayo kila mmoja anayo kwa mwenzake.

Nadia ambaye ni miongoni mwa wasanii bora wa kike nchini na kote Afrika Mashariki anadai kuwa mapenzi yao yamekabiliwa na changamoto si haba ila wamevumilia yote.

Kwa upande wake Arrow Bwoy anamuahidi Nadia mapenzi yasio na mwisho na kudai kuwa hawezi endelea kuishi iwapo Mukami atawahi muacha.

"Milima na mabonde nimepanda na kushuka na bado narudi kwako" Arrow Bwoy anamwambia Nadia kwenye wimbo huo.

Tazama video hapa:-

#ArrowBwoy #Raha #NadiaMukami THE TWO LOVE BIRDS AT IT AGAIN !! Stream The Audio; https://smartklix.com/Raha(feat.NadiaMukami) ARROW BWOY : a multi-arrow- winning Afro Dancehall artist from Kenya - is releasing his widely anticipated album. The 14- track masterpiece is titled FOCUS and it features melodic contributions from artists spawning the globe, Recorded in English, Swahili and Luganda. The Focus is a homely and reflective compilation that delivers a reflective, prophetic and encouraging experience to listeners. Arrow Bwoy linked up again with Nadia Mukami to bring you another fire collabo titled RAHA of the FOCUS album Written & Performed by: Arrow Bwoy & Nadia Mukami Audio Produced by: VickyPondis Connect with Arrow Bwoy: Bookings: samgolddave@gmail.com +254718359159 FACEBOOK https://m.facebook.com/Arrow-Bwoy-1507955109533512/ TWITTER https://twitter.com/ArrowBwoyKe?s=03 INSTAGRAM http://instagram.com/arrowbwoy

Kibao hicho kimepokewa vyema na mashabiki wao huku baadhi yao wakiwapongeza kwa mapenzi yao yanayoonekana kuwa matamu kweli.

Hata hivyo kuna wasiwasi kuwa huenda tangazo lao kuwa wanachumbiana lilikuwa kiki tu kwani sio mara ya kwanza Nadia kutambulisha mwanaume kama mpenzi wake kisha akatoa wimbo.

Mnamo mwezi Mei Nadia alitambulisha mwanaume mwenye asili ya Kihindi kwa jina Priyan na kudai kuwa alikuwa amepata kipenzi cha moyo wake.

Nadia alimshirikisha Priyan kwenye video ya kibao chake cha mapenzi  'Nipe Yote' .

Wawili hao walidhaniwa kuwa wapenzi, jambo ambalo Nadia alipuuzilia mbali wakati walipokuwa wanatangaza hadharani kuhusu uhusiano wao na Arrow Bwoy.

"Alikuwa tu wa video" Nadia alisema wiki iliyopita.

Wiki iliyopita Nadia alipuuzilia mbali madai kuwa mapenzi yake na Arrow Bwoy ni kiki na kusema kuwa amehitimu umri ambapo anataka kuanza kutengeneza familia pamoja na mpenzi wake.

" Sio kiki! naona watu hawaamini kwani kwa muda.. Hata mimi nimeanza kuzeeka, nahitimu miaka 25 mwaka huu. Inafikia wakati fulani ambapo unataka tu kufurahia maisha pamoja na mtu na unataka kujenga maisha ya usoni na mtu. Watu hawaamini, ni sawa. Hatuwezi badiliha dhana za mtu kutuhusu" Nadia alisema.