Niliachana na mpenzi wangu baada ya kuavya mimba yangu-Jamaa amwaya mtama

Muhtasari
  • Jamaa aeleza aliachana na mpenzi wake baada ya kuavya mimba yake
sad man
sad man

Je kwa nini uliachana na mpenzi wako wa awali au mke wako, nini haswa kilisababisha uhusiano wenu kuisha na kukamilika?

Nikiwa katika ziara zangu, baadhi ya watu na mashabiki walinielezea sababu ya kuachana na wapenzi wao licha ya upendo wao kunoga kila kuchao.

Mmoja wa mashabiki alieleza sababu kuu ya kuachana na mpenzi wake,na huu hapa usimulizi wake;

"Nilikuwa na mpenzi wangu amabye tulikuwa katika mahusiano kwa muda wa miaka 3, tulifanya tendo la ndoa mara kwwa mara tulipokutana

baada ya miaka 2 alibeba ujauzito wangu, licha yangu kumwambia aweke ujauzito wangu kwa maana nilikuwa natamani mtoto, aliniibia pesa zangu na akaenda kuavya mimba

Rafiki yake ndiye aliniharifu kile mwanamke huyo alikuwa amefanya, papo kwa hapo tuliachana kwa maana nilikuwa tayari kuchukua majukumu yote, na nilikuwa nimempenda sana," Alieleza Jamaa huyo.

Mwingine alikuwa na haya ya kusema;

"Mpenzi wanu alikuwa na ujauzito wa mwanamume mwingine, niliambia na rafiki yake na nikaamua kumuacha."

Byegon naye alisimulia kilichomtenganisha na mpenzi wake;

"Alama ziko zote za kimapenzi na za Vita juu nakumbuka akiniuma kwa kifua juu ya furaha tena za Vita ziko kwa miguu aliwahi nikata na chupa...... majeraha dooooh!!!"