Gavana Alfred Mutua na Rayvanny kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa njia ya kipekee Ole sereni

Muhtasari
  • Gavana Alfred Mutua na Rayvanny kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa njia ya kipekee Ole sereni

Gavana wa kaunti ya Machakos Alfred Mutua anasababu ya kutabasamu baada ya kupitia magumu,wiki hii.

Je sababu ya kutabasamu ni ipi?

Siku ya juma pili gavana huyo ataadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa njia ya kipekee,sio kuadhimisha tu bali atakuwa anasherehekea na staa wa bongo kutoka Tanzania Rayvanny, na kuweka sherehe katika eneo la Ole Sereni.

Mwezi uliopita Mutua alisafiri Tanzania na alionekana na staa huyo wa bongo, na kumpongeza kwa kazi yake nzuri.

Je utafika aje kwenye sherehe hiyo?

Ni sherehe ambayo itafanyika siku ya Jumapili, Agosti 22 katika hoteli ya Ole Sereni,kama wataka kuhudhuria sherehe hiyo haya basi sikiza Radiojambo, na kujibu maswali boga zaidi ujishindie tiketi.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook Mutua alikuwa na haya ya kusema;

"Jumapili, Agosti 22, ni siku yangu ya kuzaliwa na pia siku ya kuzaliwa ya Rayvanny - Tumeamua kufanya sherehe maalum ya kuzaliwa mara mbili kwa watu wachache Jumapili alasiri. Tafadhali pata tikiti yako ya bure na ujiunge nasi kwa chakula na muziki," Aliandika Mutua.

Haya basi usikose!