"Wanaume wa aina hii hawako tena" Akothee ashauri Jacque Wolper namna ya kutunza mumewe baada ya kuvishwa pete

Akothee amewapongeza wawili hao na kumsifia sana Rich Mitindo kwa mapenzi makubwa ambayo ameonyesha mkewe.

Muhtasari

•Mwigizaji Jacqueline Wolper alivishwa pete ya uchumba na mpenzi wake wa sasa Rich Mitindo katika hafla iliyopambwa kweli.

•Miongoni mwa wale ambao wameonekana kumezea mate hatua ya Wolper kuvishwa pete ni mwanamuziki na mfanyibiashara mashuhuri nchini Kenya Esther Akoth almaarufu kama Akothee.

Akothee, Rich Mitindo, Jackie Wolper
Akothee, Rich Mitindo, Jackie Wolper
Image: INSTAGRAM

Wikendi iliyopita, aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki Harmonize, mwigizaji Jacqueline Wolper alivishwa pete ya uchumba na mpenzi wake wa sasa Rich Mitindo katika hafla iliyopambwa kweli.

Wolper ambaye alionekana mwenye bashasha si haba alisema kuwa Mungu alikuwa amemtimizia ndoto yake ya pili baada ya kujaliwa mtoto. 

Wengi wameendelea kuwasherehekea wanandoa hao wawili na kuwapongeza kwa hatua kubwa waliyochukua maishani mwao.

Miongoni mwa wale ambao wameonekana kumezea mate hatua ya Wolper kuvishwa pete ni mwanamuziki na mfanyibiashara mashuhuri nchini Kenya Esther Akoth almaarufu kama Akothee.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Akothee amewapongeza wawili hao na kumsifia sana Rich Mitindo kwa mapenzi makubwa ambayo ameonyesha mkewe.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa wanaume kama wale ni nadra sana kupatikana siku hizi na kusema kuwa akapata wa kumuonyesha mapenzi kama yale anaweza patwa na furaha kubwa isiyoelezeka. Akothee amemshauri Wolper kumtunza na kumdekeza mumewe akisema kuwa wanaume kama wale hawapo tena.

"Siku kijana wa pharaoh atanifanyia hivi mimi sitaposti.. nitaenda kutembea dunia kwanza niposti nikirudi.. ile furaha nitakuwa nayo, hata simu nitapasua..@wolperstylish huyu mume, babake mtoto wako wa kwanza , mtunze, mdekeze, akija nyumbani amechoka mpe massage.. akitaka kwenda chooni angalia kama kuna tissue,baby asiteseke. Ukiona ako na pressure kidogo mpe pesa hata kama ako nazo.

Yaani kwa upole, wanaume wa aina hii, hawako tena, na kama wako basi ni wawili waatu, mtunze mumeo @richmitindo.

Na wewe Baba P umecheza kama wewe, hongera, mtunze mkeo, yeye ni ua, maji, mbolea, mchanga, utajua wewe.. Hongera saana wapenzi" Akothee alisema.

Mwigizaji Wolper kwa upande wake alimshukuru Akothee kwa  upendo wake na ushauri na kuahdi kuwa ataufuata.

"Au niite press bby waaaaa i love u my friend u that yah nakupenda na Asante sanaa kwa upendo wakila siku nahayo mashauri hapo nitayafwata nakuyazidisha pia mana nataka niweke pia mgongo akule na ashibe chakula kikiwa mgongoni" Wolper alimjibu Akothee.