Hutuwezi endelea kupoteza maisha kwa ajili ya kafyu,'Mchekeshaji MCA Tricky alaani unyama wa polisi

Muhtasari
  • Mchekeshaji MCA Tricky alaani unyama wa polisi
  • Polisi wanadaiwa kumpiga jamaa mmoja hadi kifo kwa kukiuka amri ya kutotoka nje iliyowekwa kudhibiti maambukizi ya Corona
Maandamano Kayole
Image: Hisani

Maandamano yameshuhudiwa  siku ya Alhamisi katika mtaa wa Kayole wakazi wakilalamikia mauaji ya kiholelaholela yanayodaiwa kutekelezwa na maafisa wa polisi dhidi ya mmoja wao usiku wa Jumatano.

Polisi wanadaiwa kumpiga jamaa mmoja hadi kifo kwa kukiuka amri ya kutotoka nje iliyowekwa kudhibiti maambukizi ya Corona.

Tukio hilo lilitokea maeneo ya Tushauriane wakati marehemu alikuwa anaelekea nyumbani kwake.

Inaripotiwa kuwa mhasiriwa alikuwa amearifu mkewe kuhusu mateso aliyokuwa anapitia mikononi mwa askari waliokuwa wamemkamata  na hata kumtumia nambari ya gari lililokuwa limembeba.

Haya yanajiri wiki chache baada ya polisi Embu, kudaiwa kuwauwa ndugu wawili Emmanuel na Benson kwa kukiuka amri ya kutotoka nje.

Polisi hao walichukuliwa hatua na kuzuiwa kwa muda wa siku 14 ili uchunguzi ukamilike, sio mmoja au wawili bali baadhi ya wakenya wamewapoteza wapendwa wao baada ya kupitia mikononi mwa polisi.

Wakenya,wanamitandao,watu mashuhuri miongoni mwa wenine wanataka unyama wa polisi ukamilike.

Mchekeshaji wa churchill MCA Tricky kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amedai kwamba watu na wakenya hawatazzidi kupoteza maisha yao kwa ajili ya kafyu.

Pia ametaka ukatili, unyama wa polisi ukamilike haraka iwezekanavyo.

"#Kayole Polisi wanapaswa kuheshimu haki ya maisha, hatuwezi endelea kupotea maisha kwa ajili ya visingizio za amri ya kutotoka nje," Aliandika Tricky.

Wanamitandao walimuunga mkono na hizi hapa baadhi ya jumbe zao;

blacshady: So true vijana wanaisha😢😢

gounah23: Brutality must stop

samerigideon: La sivyo hata sisi tutaanza kuwa brutal kwao.

karenjonyunsuu: Together tukomeshe 😢

ronnyreagan5: SAY NO TO POLICE BRUTALITY. ENOUGH IS ENOUGH. ARISE YOUTHS AND FIGHT FOR WHAT YOU BELIEVE IN.