Mfahamu Grand P, Bilionea aliyevunja vikwazo vyote na kuchumbia mwanadada mnene mara kadhaa zaidi yake

Inaaminika kuwa alizaliwa mwezi Oktoba mwaka wa 1993 na alizaliwa na hali ya kimaumbile inayofahamika kama Progeria ambayo ilizuia mwili wake kuwa mkubwa.

Muhtasari

•Wengi wanamfahamu Grand P kama bilionea mashuhuri mwenye maumbile madogo ya kipekee naye Eudoxie yao kama mwanasoshalaiti mashuhuri  aliyebarikiwa na umbo wa kumezewa mate na wanaume wengi.

Grand P na Eudoxie Yao
Grand P na Eudoxie Yao
Image: INSTAGRAM

Grand P na mpenzi wake Eudoxie Yao ni wanandoa ambao wamezungumzia sana katika kipindi cha wiki kadhaa zilizopita.

Kutengana kwa wawili hao takriban wiki tatu  zilizopita kuliibua mdahalo mkubwa sana mitandaoni kote bara Afrika na wameendelea kuvuma hadi kurudiana kwao ambako kulifichuka hivi majuzi.

Wengi wanamfahamu Grand P kama bilionea mashuhuri mwenye maumbile madogo ya kipekee naye Eudoxie yao kama mwanasoshalaiti mashuhuri  aliyebarikiwa na umbo wa kumezewa mate na wanaume wengi.

Image: INSTAGRAM// GRAND P

Lakini wawili hao ni kina nani haswa? 

Moussa Sandiana Kaba almaarufu kama Grand P ni mwanamuziki, mwigizaji na mwanasiasa tajiri siasa tajiri sana nchini Guinea.

Inaaminika kuwa alizaliwa  mwezi Oktoba mwaka wa 1993 na alizaliwa na hali ya kimaumbile inayofahamika kama Progeria ambayo ilizuia mwili wake kuwa mkubwa.

Machache sana yamezungumziwa kuhusu maisha yake ya awali haswa kuhusu masomo yake ingawa inasemekana kuwa msanii huyo alikejeliwa sana kutokana na maumbile yake katika maisha yake ya utotoni.

Msanii huyo pia ameficha familia yake hadharani na machache sana yanafahamika kuhusu asili yake.

Alianza taaluma yake ya usanii zaidi ya miaka kumi iliyopita na ameorodheshwa kama mmoja wa wasanii wakubwa nchini Guinea.

Grand P alikuja kufahamika zaidi na kupata umaarufu mkubwa zaidi duniani alipoanza kumchumbia mwanasoshalaiti Eudoxie Yao kutoka Ivory Coast.

Alishangaza wengi alipotangaza azma yake ya kugombea kiti cha urais kwenye uchaguzi ujao.

Eudoxie Yao amejaribu kuweka umri wake halisi kwa usiri ila inaaminika kuwa alizaliwa miaka ya 80's. Yeye huadhimisha siku yake ya kuzaliwa mwezi Juni.

Mwanadada huyo ambaye anasifiwa sana kufuatia umbo wake wa kipekee alizaliwa jijini Abijan huko Ivory Coast. 

Alipata umaarufu mkubwa kufuatia picha za kuvutia alizopakia kwenye mitandao ya kijamii ambako ana ufuasi mkubwa kweli.  Kufikia sasa Yao ana wafuasi milioni 1.6 kwenye mtandao wa Instagram na wafuasi milioni 5.3 kwenye mtandao wa Facebook.

Anajulikana kwa jina la kitani kama 'Kim Kardashian wa Afrika' kutokana na maumbile yake.

Kando na ushawishi wake mitandaoni, Yao pia ni mwanamitindo na mwanamuziki mashuhuri magharibi mwa Afrika.

Alipata umaarufu zaidi alipoanza kuchumbiana na bilionea Grand P.