'Wewe ni mume bora kwangu,'Mama Dangote amwandikia mumewe ujumbe wa mahaba

Muhtasari
  • Mama Dangote amwandikia mumewe ujumbe wa mahaba
sandra 1
sandra 1

Mama wa msanii maarufu wa bongo Diamond Platinumz, Sandra maarufu kwa jina la Mama Dangote na wafuasi wa mtoto wake, amekuwa akivuma muda kwa muda kwenye wanablogu Tanzania kwa ajili ya maisha yake ya mapenzi.

Licha ya hayo, kuwa mama mmoja na aliyefanikiwa maisha yake ya mapenzi yamemfanya avume sana, na kuzungukwa na drama.

Naam, kulingana na hadithi yake ya mapenzi, aliachwa kulea watoto wake peke yake katika umri mdogo sana.

Pamoja na uzoefu huu, aliapa kwamba hataruhusu chochote kizuie mafanikio ya watoto wake.

Baada ya kukaa mseja kwa ajili ya watoto wake, Sandra aliamua kupata mwanamume wa kumuita mume. Nia yake ilimpeleka mikononi mwa Uncle Shamte

Kupitia kwenye ukurasa wke wa instagram Mama Dangote alimwandikia mumewe Shamte ujumbe wa mahaba, na kumsifia.

"SI RAFIKI TU.!! WEWE NI MUME BORA KWANGU MAISALA ..NAKUTAKIA MAISHA MAREFU YENYE BARAKA TELE @uncle_shamte ❤," Aliandika Mama Dangote.

Hizi hapa hisia za mashabiki;

testar_baddest: Vipi kuhusu watoto au ndio mmeghahili

lungimaulanga: Sanaaaa mpende akupedae🔥🔥🔥

alhajj_seif: Hbd brother Uncle Shamte Allah akujaalie maisha marefu zaidi Inshaallah!

mkamatimbisi: Huyu Auncle Mungu akutunzie tu maana kwa muonekano tu Ana busara nyingi sana hata walikuwa wanapiga kelele wote kimya! Munhu aendelee kuwatunza @mama_dangote

dineygabbydrisa:❤️❤️nikiwa mkubwa nataka kupendwa kama wewe😂