'Mbele iko sawa,'Gavana Mutua asema baada ya kuulizwa apatanishwe na mkewe

Muhtasari
  • Mutua ajibu haya baada ya kuulizwa apatanishwe na mkewe
Image: INSTAGRAM//GOVERNOR ALFRED MUTUA

Gavana wa Machakos Alfred Mutua anatazamia kuwa na siku ya kipekee JUmapili Agosti 22, kwa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa na msanii wa bongo Rayvanny.

Wiki jana gavana huyo alivuma mitandaoni baada ya kutengana na mkewe.

Akiwa kwenye mahojiano siku ya Ijumaa na mpasho aliwashauri wapenzi wote wakiachana wanapaswa kuachana kwa amani.

"Mimi ni muumini wa mapenzi na kwamba mtu hapaswi kamwe kukata tamaa bila kujali kila kitu

Sherehekea kila wakati watu wanaoingia maishani mwako, kila wakati uwe na uhusiano mzuri na watu wanaoingia maishani mwako.

Naona vijana wanakosana wanatukanana na kupigana, ni ujinga,Ikiwa umewahi kupenda na mtu mapenzi hayapotei, watendee wengine kwa fadhili," Aliazungumza Mutua.

Akiwa kwenye studio za Radiojambo Ijumaa asubuhi, mtangazaji Gidi alimuuliza kama angependa kupatanishwa na mkewe.

"Mheshimiwa patanisho je?" Gidi alimuuliza Mutua.

Gavana huyo alijibu na kusema;

"Mbele iko sawa,"

“Mbele iko sawa....” Alfred Mutua. Asema Dr. Alfred Mutua baada ya kuulizwa na GIDI GIDI na Ghost Mulee kama atapatanishwa na mkewe. #GidiNaGhostAsubuhi #OngeaUsikike

Posted by Radio Jambo on Friday, August 20, 2021

Hizi hapa baadhi ya hisia za mashabiki wa Radiojambo baada ya Mutua kumjibu Gidi;

Sk Lagat: Patanisha Mutua na Lilian on monday

Alexhy Muah: Mjamaa analia kw roho lkni anaonyesha tu furaha bure

Veronica Maloba: Mutua tunakuombea,c wote wanafurahia kukiwa na furaha kwenye ndoa,be prayerful

Robai Shamagoi: Songa mbele Mutua wee si Wa Kwanza achika tu Na utafute akupendaye

Baraka Halfan: Naoma ma single wako na governor sasa,,mbele iko sawa pamoja😅🤣

Sandy E. Shandy: Mutua still strong dispite kuwachwa🤣🤣

Kale Dota: Si mungepatanishwa tu