Penda mtu ambaye unahisi uko salama naye-Muigizaji Brenda Wairimu awashauri mashabiki

Muhtasari
  • Muigizaji Brenda Wairimu awaonya mashaiki wake kuhusu mapenzi

Muigizaji Brenda Wairimu alifahamika sana kupitia kwenye kipindi cha Monica kilichokuwa kinapeperushwa kupitia kwenye runinga ya Maisha Magic East.

Je umewahi penda mtu lakini unaoana kwamba mapenzi yako hayatoshi lazima ufanye jambo ili mpenzi wako aone kuwa unampenda?

Kuna baadhi ya watu ambao hujuta kwanini waliwapenda wenzi wao kwani huwa wanahitaji kuthibitisha mapenzi yao kwao.

Naam,muigizaji Brenda amewashauri mashabiki wake kuwa wanapaswa kuoenda mtu ambaye wanahisi kuwa salama nao.

"Hauwezi mpenda mtu ambaye anayekupa vipepeo ... hiyo ni njia ya miili yako kukuambia mambo mabaya, una wasiwasi, unaogopa .. wananipenda ... wananipenda .. wananipenda ... unakuwa mraibu wa mapenzi yao, idhini yao, kwa sababu unataka hisia hiyo tena kifuani mwako. Kuanguka kwa upendo na mtu anayekufanya ujisikie salama, anayekufanya uwe na utulivu, ndiye mtu unayempenda,"Alishauri Brenda.

Ujumbe wake na ushauri wake unajiri wiki moja baada ya kuvuma sana mitandaoni kwa kusema kwamba alidanganywa na aliyekuwa mpenzi wake.

Baadhi ya wanamitandao walidai kwamba ni aliyekuwa mpenzi wake JUliani, lakini alijitokeza na kukana madai hayo.