'Nitaoa kwa wakati ufaao,'Mwanahabari Trevor Ombija azungumzia kuoa

Muhtasari
  • Mwanahabari a runinga ya Citizen Trevor Ombija ni miongoni mwa wanahabari ambao wana talanta ya kazi yao
  • Ombija anafahamika sana kwa kazi yake, na vile anaishi maisha yake
Trevor Ombija
Image: Instagram

Mwanahabari a runinga ya Citizen Trevor Ombija ni miongoni mwa wanahabari ambao wana talanta ya kazi yao.

Ombija anafahamika sana kwa kazi yake, na vile anaishi maisha yake.

Akizungumza na Kalondu Musyimi, Ombija alisema kwamba  yeye ni muumini wa ndoa na anajua kuwa inaweza kufanya kazi wakati wote ikiwa wenzi wote wako ndani ya hiyo ndoa.

"Ni juhudi za makusudi kutoka kwa nyinyi wawili, nyinyi wawili mnapaswa kuwa tayari kukubaliana, kuzungumza, ina kazi nyingi.

Haipaswi kuwa mtu mmoja anaweka asilimia ya 40% na mwingine  asilimia ya 60%, ninyi nyote mnapaswa kuwa 50-50. Maelewano ndio jambo kubwa katika ndoa, "Alieleza Ombija.

Pia alifichua kuwa kwa sasa hana haraka ya kuoa, lakini anatarajia kufanya hivyo wakati mzuri utakapofika.

"Nitafanya hivyo, kwa wakati unaofaa, na mtu sahihi. Muniombee!"

Ombija alifichua pia kwamba DM yake imejaa wanawake ambao ni warembi bali anawajibu yuko sawa.

Alizungumia uhusiano aliokuwa nao miaka 10 iliyopita, na hata kulipa mahari lakini mambo hayakuenda sawa.

Je unaweza pata mwanamume mwanifu kweli, ambaye anatumiwa jumbe na wanwake lakini anawapuuza?