Sikuwahi kufikiria siku moja nitachukua kipazasauti na kuhubiri-Size 8

Muhtasari
  • Msanii wa nyimbo za injili Size 8 amewaacha mashabiki wake, na hisia za mhemko baada ya kumshukuru Mungu kwa umbali amemtoa
  • Wengi wanafahamu safari ya Size 8 ya muziki, kwani alianza kuimba nyimbo za Secular kisha akaanza za injili

Msanii wa nyimbo za injili Size 8 amewaacha mashabiki wake, na hisia za mhemko baada ya kumshukuru Mungu kwa umbali amemtoa.

Wengi wanafahamu safari ya Size 8 ya muziki, kwani alianza kuimba nyimbo za Secular kisha akaanza za injili.

"Maneno hayawezi kuonyesha shukrani zangu kwa Mungu nimeona rehema zake maishani mwangu 😭😭😭😭

Nilikuwa msichana kutoka ulimwenguni akiimba muziki wa kidunia lakini Mungu kwa huruma yake aliniokoa kupitia Yesu Kristo na kunisafisha Alinihesabia haki na sasa alinistahilisha kufanya mapenzi yake. Sikuwahi kufikiria siku moja nitachukua kipasa sauti na kuhubiri 😳 ni kama sinema ...

Waaa Mungu amejaa mshangao na anaweza kutumia yoyote Atakayochagua, huu ni mwanzo wa safari mpya ambayo sistahili. hii, ni kwa neema na rehema za Mungu tu yeye mwenyewe ameifanya kupitia mimi !!!" Alisema Size 8.

Alizidi na kuwashauri mashabiki wake kwamba hawapaswi kubatilishwa na mtu kwani Mungu humtumia mtu yeyote kwa vyovyote.

Pia alishindwa ni upendo gani Mungu amempenda, kwani ameona hukuu wake.

Watu wanaweza kukubatilisha lakini Usijibatilishe mwenyewe Mungu hutumia mtu yeyote na kwa vyovyote atakavyochagua,

Mungu alimchagua Paulo mtume ambaye alikuwa akiua Wakristo na kumgeuza kuwa mtume mkuu.

Yeye ndiye Elohim Bwana aliye huru hakuna lisilowezekana pamoja Naye. Na kwa Mshauri wangu Nabii Kelvin Ephraim woi Mungu akubariki milele bila kutokunihukumu kwa sababu ya zamani lakini akiangalia siku zangu za usoni na siku zote anazungumza na maisha katika nuru ya Mungu.

😭😭😭 YEHOVA MUNGU NI NAMNA GANI YA UPENDO HII UMENIPENDA SANA ❤️ ♥ ️💖 !!! NIPO KATIKA AWE YAWEH !!! 😭😭😭 SIAMINI MACHO YANGU !!! MUNGU ANAWEZA KUWEZA !!"