Msanii Jose Chameleone apata nafuu siku chache baada ya kulazwa

Muhtasari
  • Msanii kutoka Uganda Jose Chameleone anapata afueni baada ya kulazwa hospitali siku chache zilizopita

Msanii kutoka Uganda Jose Chameleone anapata afueni baada ya kulazwa hospitali siku chache zilizopita.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Jose alipakia picha akiwa  kwenye kitanda cha hospitali, na kumshukuru mama yake kwa kuwa naye wakati huu mgumu na kwa hali yoyote.

"Asante Mama, upendo wako ni dhahiri. Hujawahi kuacha juu ya ukweli! Nitakua kujifunza kwa nguvu kutoka kwako. Mungu atakupa maisha zaidi 🙏 "alishiriki Jose Chameleone.

Chapisho linakuja siku chache baada ya kuripotiwa kuwa mwimbaji alikuwa amelazwa Hospitali ya Nakasero huko Kampal

Kwa mujibu wa mkewe Daniella Atim, Jose anasumbuliwa na helikobacter pylori (H. pylori). Daniella, ambaye anaishi Marekani na watoto wao watano, aliwaambia wanamitandao kuacha kupakia picha za Chameleone kwa sababu zinaweza kuathiri watoto wake.

Hizi hapa baadhi ya jumbe za wanamitandao wakimtakia afueni ya haraka;

akotheekenya: Joseee ,Mungu akulinde Legend ,we love you

mainawakageni: Get well soon Brother... quick recovery!!!! We are here for you, my legend

presenter001: Pole sana, may God heal you and bless your mama

kingast: Mungu anakupenda na endelea kumuamini yeye ndio mponya kwa kila ugonjwa na kila Jambo tunakuombea mwenyezi mungu akuponye na akupe afya njema na maisha marefu

uzeelelia: Pole sana Jose Mungu akulinde upone haraka nimeumia sana kupata taarifa kwamba unaumwa nyimbo zako huwa zinanifariji nikiwa nyumbani ama kazini.

fauziasamantha99: Quick recovery papa🙏🙏🙏