logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Nakupeza sana sikujua kama utatuacha ghafla,'Mwanawe seneta mteule Prengei amuomboleza

Prengei alifariki wiki iliyopita baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani

image
na Radio Jambo

Burudani26 August 2021 - 10:07

Muhtasari


  • Mwanawe seneta mteule Prengei amuomboleza
  • Prengei alifariki wiki iliyopita baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani katika eneo la Gioto katika Kaunti ya Nakuru
Marehemu Victor Prengei

Valarie Prengei, binti wa seneta mteule marehemu Victor Prengei aliwaacha waombolezaji kwa machoozi baada ya kumsifu baba yake na kusema jinsi anampeza.

Ujumbe wake wa kumuomboleza baba yake ulisomwa wakati wa ibada ya wafu ya Marehemu Victor Prengei iliyofanyika katika kanisa la Good shepherd Alhamisi 26/08/2021.

Prengei alifariki wiki iliyopita baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani katika eneo la Gioto katika Kaunti ya Nakuru.

"Baba nakukosa na kukupeza  sana, sikujua kamwe utatuacha ghafla sana,Ulikuwa baba mzuri, ulinishauri na ukafanya bora kutulinda  mimi na ndugu zangu.

Ninaahidi kuendelea na masomo yangu kama vile ulivyotaka. Ulijaribu kadri ya uwezo wako kusaidia watu na jamii kwa jumla bila mipaka.

Nilikuwa na huzuni wakati nilisikia juu ya kifo chako. Mungu alisema katika vitu vyote tunapaswa kumthamini. Kifo chako kiliacha kovu mioyoni mwetu lakini urithi wako utasimama maishani mwetu milele.Tutakupeza, baba. "

Kulingana na Catherine Prengei, mke wa seneta aliyekufa. Leo pia ni siku ya kuzaliwa ya mtoto wao.

Kutoka kwetu wanajambo Mungu azidi kuilaza roho yake mahali pema peponi.

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved