'Moyo wangu umeng'olewa kutoka kifuani,' Larry Madowo ampoteza nyanya yake

Muhtasari
  • Mwanahabari wa CNN Larry Madowo kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram ametangaza kifo cha nyanya yake
madowo1
madowo1

Mwanahabari wa CNN Larry Madowo kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram ametangaza kifo cha nyanya yake.

Katika chapisho kwenye mitandao yake ya kijamii, Madowo alimtaja bibi yake kama kiongozi wa familia yake.

"Bibi yangu, mchungaji wa familia, mapigo ya moyo wetu, mwenzi wangu wa ucheshi, mpendwa Francesca Madowo amejiunga na mababu.

Nimepata ganzi. Moyo wangu umeng'olewa kutoka kifuani. Nuru imetoka maishani mwangu. Nind gi kwe, min Omollo," ilisomeka barua hiyo," Aliandika Madowo.

Hizi hapa baadhi ya jumbe za rambi rambi kutoka kwa mashabiki wake;

henrydesagu: Our deepest condolences may Grandma Rest in Peace

juliegichuru: So sorry Larry. She is resting 🙏

globemich: Lots of love and strength to you my friend. She was such sweet soul. Will never forget her kindness and her amazing smile.❤️

bonifacemwangi: Pole Sana my brother. May the good Lord comfort you and your well. Go well Cucu.

macksjuma: Rest in peace grandma 😢