'Huwa nabusu familia yangu kila asubuhi na jioni kwani huenda ni mara ya mwisho nawaona' Mwanaharakati Boniface Mwangi azungumzia familia yake

Mwanaharakati mashuhuri Boniface Mwangi amefunguka kuhusu uhusiano katika familia yake na jinsi yeye huitunza.

Muhtasari

•Kupitia ukurasa wake wa Instagram, baba huyo wa watoto watatu amekiri kuwa yeye hubusu mkewe na watoto wake kila asubuhi  na jioni kabla ya kulala kwani huenda ikawa mara ya mwisho yao kuonana.

Image: INSTAGRAM// BONIFACE MWANGI

Mwanaharakati mashuhuri Boniface Mwangi amefunguka kuhusu uhusiano katika familia yake na jinsi yeye huitunza. 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, baba huyo wa watoto watatu amekiri kuwa yeye hubusu mkewe na watoto wake kila asubuhi  na jioni kabla ya kulala kwani huenda ikawa mara ya mwisho yao kuonana.

Isitoshe, mwanaharakati huyo amefichua kuwa walikubaliana na mkewe kuwa licha ya mzozo wowote kati ya ni sharti wakumbatiane kila usiku wanapolala ila hakuna kushiriki mapenzi kama hawajasuluhisha mzozo ulioko.

"Mimi hubusu mke na watoto wangu kila asubuhi na jioni. Tulikubaliana na mke wangu @njerikan kuwa bila kujali mzozo na mambo yanayokuja kati yetu, lazima tunakumbatiana kila usiku (hakuna kushiriki mapenzi kama bado kuna mzozo hatujasuluhisha). Huwa tunabusu kwaheri kila asubuhi na kuambiana karibu nyumbani kila mmoja wetu anapoingia kwa nyumba. Huwa tunabusu watoto wetu angalau mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni. 'Nakupenda' ni lugha yetu ya kila siku." Mwangi alisema.

Mwanaharakati huyo ambaye pia ni mwanahabari amefunga pingu za maisha na Hellen Njeri na pamoja wamebarikiwa na watoto watatu; Simphiwe, Sifa na Mboya.