Kesi ya R. Kelly: Mwathiriwa wa kiume atoa ushahidi wa unyanyasaji wa kingono

Bwana Kelly, 54, amekanusha mashtaka yote dhidi yake.

Muhtasari

•.Mwanamume huyo aliyetoa Ushahidi kwa kutumia jina la kisiri la Louis, alisema alikuwa na miaka 17 wakati Bwana Kelly alipomuuliza "yuko tayari kufanya nini kwa ajili ya muziki".

•Aliiambia mahakama kuwa Bw. Kelly alimpatia namba ya simu na kumkaribisha nyumbani kwake, akisema angeweza kutumbuiza katika studio ya kurekodi na kupokea vidokezo kadhaa kwenye biasharaya muziki.

Image: GETTY IMAGES

Kesi ya msanii R. Kelly kuhusu unyanyasaji wa kingono imeingi asiku ya nane Jumatatu , huku mlalamishi wa kiume akitoa Ushahidi kwamba nyota huyo wa muziki alimuahidi umaarufu akikubali kufanya ngono naye.

Mwanamume huyo aliyetoa Ushahidi kwa kutumia jina la kisiri la Louis, alisema alikuwa na miaka 17 wakati Bwana Kelly alipomuuliza "yuko tayari kufanya nini kwa ajili ya muziki".

Kisha akelezea jinsi mwanamuziki huyo alivyotambaakuelekea kwake akifanya onyesho la kimapenzi , ijapokuwa "sikutaka kujihusisha na hayo".

Bwana Kelly, 54, amekanusha mashtaka yote dhidi yake.

Hii ni pamoja na hshtaka moja la udanganyifu - ambayo inamuonyesha kama mkuu wa biashara ya jinai ambayo lengo lake lilikuwa "kuwateka wanawake wadogo na vijana" kwa madhumuni ya ngono - na makosa manane ya kukiuka sheria ya biashara ya ngono inayojulikana kama Sheria ya Mann.

Mwimbaji huyo ambaye jina lake kamili ni Robert Kelly, hajashtakiwa kwa ubakaji na kushambulia, lakini waendesha mashtaka wanaruhusiwa kutoa ushahidi wa uhalifu wowote unaohusiana na mashtaka ya ujambazi, bila kujali ni lini ulitokea.

Aliiambia mahakama kuwa Bw. Kelly alimpatia namba ya simu na kumkaribisha nyumbani kwake, akisema angeweza kutumbuiza katika studio ya kurekodi na kupokea vidokezo kadhaa kwenye biasharaya muziki.

Siku ya Jumatatu, majaji walisikia ushahidi wa waathiriwa wawili, wote wanasema walikuwa watoto wakati walipokutana na na Bw.Kelly.

Louis alisema alikutana mara ya kwanza na Bw. Kelly mwaka 2006, akiwa na miaka 17-akifanya kazi nyakati za usiku katika McDonald's mjini Chicago.