Msanii Mercy Masika amsifia mumewe huku wakiadhimisha miaka 13 kwenye ndoa

Muhtasari
  • Msanii Mercy Masika amsifia mumewe huku wakiadhimisha miaka 13 kwenye ndoa
Mercy Masika's Husband
Mercy Masika's Husband

Msanii wa Injili Mercy Masika kwa ujumla ni mmoja wa wanamuziki wa injili thabiti kabisa katika tasnia ya muziki, ambaye licha ya changamoto wanamuziki wanaopitia kwenye tasnia hii leo ameweza kuzishinda na akaendelea kuwa muhimu katika tasnia hiyo.

Yeye sio mwanamuziki tu bali pia ni mke  na ana mwanamume ambaye anamthamini sana na wameishi pamoja kwa zaidi ya miaka 13 sasa.

Kupitia kwenye ukurasa wkae wa instaram huku wakiadhimisha miaka 13 kwenye ndoa, alimsifia mumewe na kumhakikishia angemuoa tena.

"Maadhimisho ya miaka 13 kwetu. Ninajiona kuwa mwenye heri kufanya maisha na wewe Han. Upendo wako umeniumba na kunitia nguvu

Kwa kweli bado ningekuoa tena ikiwa kuna maisha ya pili kwa sababu umempenda Hekima. Asante kwa miaka 13 ya kushangaza," Aliandika Mercy.

Wanandoa hao wamebarikiwa na watoto 3 pamoja.